NGUVU YA KUSIMAMA KATIKA NAFASI YAKO-5
...INAENDELEA
Ukijua nafasi yako
unapata utulivu fulani wa ajabu ambao unakwambia Mungu ndio utoshelevu wako.
In your position,
no competition.
Mtoto asiyejua
NAFASI yake kwa baba yake hana tofauti
na mtumwa. Ni heri mtumwa
Mhubiri
10:7-HIKI NDO
KIWANGO CHA JUU KABISA CHA KUKAA NJE YA NAFASI,UTAKUWA KAMA OMBAOMBA NA HUKU
BABA YAKO ANAMILIKI VYOTE.
Mhubiri 10:7
7 Mimi nimeona
watumwa wamepanda farasi, na wakuu wakienda kwa miguu juu ya nchi kama watumwa.
Ona Mhubiri
10:6
6 ya kuwa upumbavu
huwekwa mahali pa juu sana, nao wakwasi hukaa mahali pa chini.
Mungu akupe hatua
Akuhamishe mahali
ulipo
Akupeleke
unapostahili,sio tu unapotaka
Ukigundua umetoka
nje ya NAFASI fanya TOBA NA KUOMBA REHEMA.
Jifunze utofauti
wa TOBA NA REHEMA.
Wengine mmezifanya
familia zenu kuwa masikini na ombaomba kisa hamtaki kusimama ktk nafasi zenu
SIMAMA MAHALI
PALIPOBOMOKA
Maombi mepesi na
rahisi kujibiwa na Mungu ni TOBA NA REHEMA.
Sijasema usiache
kazi au usihame...MBINGU ZIMEKUBALI?? UMERUHUSIWA??
Stay in your
position
Stand in your
position
If you are a
woman, your position is not the assistant but a helper. Assistants can overflow
their bosses, not you.
Kudai haki nje ya
nafasi yako ni kujiumiza
Haki sawa kwa wote
wakati wanaodai wenyewe hawako sawa?
Huwezi kuijua haki
yako kama uko nje nafasi yako
Kusimama imara
kwenye nafasi isiyo yako ni kujivuruga.
Usikubali kuoa na
hujui nafasi yako
Unakubalije
kuolewa na hujui nafasi yako?
Mtaenda kuanza
kugombania nafasi mpaka mmemalizana
Kaa kwenye nafasi
yako bana
Usipojua nafasi
yako kwa mtu utaishi kwa kujistukia sanaaaaa
Bwana Yesu
akawaambia wanafunzi wake....SIWAITI TENA WATUMWA...au kwa lugha ingine
NAWAHAMISHA NAFASI YENU..FROM WATUMWA TO FRIENDS...ukihamishwa nafasi hata
marupurupu yanahama na kuongezea au kupungua pia
MUNGU AKUFUNGUE
MACHO
Watu wengi sana
tuna alama ya KOSA LA LUTU/LOTI
Ukiwa kwenye
nafasi isiyo sahihi ni rahisi sana kukutana na watu wasio sahihi
Ukiwa kwenye
nafasi isiyo sahihi ni rahisi sana kuwa kwenye eneo lisilo sahihi
Wrong
position-wrong people-wrong places
Lutu alitumia
macho yake ya mwilini kuamua upande upi wa kwenda
Lutu aliongozwa na
mazingira kama wenzangu na mimi ambao huwa wanaongozwa na mazingira,
wakipangiwa kazi vijijini wanaona kama watachelewa kuendelea...NI HERI UPANGIWE
KIJIJINI NA MUNGU PAMOJA NAWE kuliko kujipangia mjini bila Mungu.
Nakumbuka
nilipokuwa nahamia Dodoma, tokea Arusha khaaaaaaaaaa nilionekana kama mpinga
Kristo...back in 2011...watu wanaingalia Dodoma wanaona kama nini sijui...lakini
nikagundua shida kubwa ni vile watu HULINGANISHA...waliiangalia Dodoma kwa
macho ya Arusha...hivo sivyo watu wa Mungu wanavyoangalia mambo.
Hatuendi kwa kuona
au kusikia.
Tunaenenda kwa
imani-hakika ya mambo ninayotarajia-bayana ya yale ambayo bado sijayaona kwa
macho
Macho haya
yanakosesha sana kwenye maeneo mengi sana...
EDEN-Hili lilikuwa
eneo sahihi kwa Adam na Eva. Eneo sahihi, nafasi sahihi.
Walipotoka tu
kwenye nafasi yao, wakaondolewa hata eneo-location.
Kuna watu wanaishi
kwa kutangatanga sanaaaaaaaa
Hawatuliii, watu
wanahisi WAMELAANIWA....
Wanaenda kuombewa
na MANABII NA MITUME waliopotoka ili kuvunja LAANA .na kumbe kumbe mtu
kajilaani mweyewe kwa kuwa yuko NJE YA NAFASI....
Anaombewa weeeeeeeeeeeee,
miaka nenda rudi… KUOMBEWA NA UKO KWENYE NAFASI ISIYO YAKO NI KUMFAIDISHA
ANAEKUOMBEA maana wewe unakuwa huna akili zako tena....
Kabala ya kuombewa
upate mume sahihi ni lazima uwe kwenye nafasi sahihi...yaani uwe na ufahamu sahihi
wa wewe ni nani mbele za Mungu.
Kabla hujaenda
kuombewa kwenye jambo lolote,jiulize...niko kwenye nafasi yangu....ama sivyo
toba na rehema inakuhusu sana.
Kiwango cha
kukosea ukiwa ndani ya nafasi yako hakifanani na kama ukiwa nje ya nafasi yako.
ITAENDELEA...
Hakuna maoni: