Ads Top

NGUVU YA UFAHAMU SAHIHI-1



NGUVU YA UFAHAMU SAHIHI

Somo letu la utangulizi linahusu NGUVU YA UFAHAMU SAHIHI

UFAHAMU SAHIHI una nguvu sana.
Ufahamu sahihi una nguvu kwa kiwango ambacho mtu asiekuwa nao anaweza kuishi kama mtumwa na huku baba yake ni Mfalme.
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa...hii inatoka Hosea 4:6
”Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.”

UFAHAMU sahihi unatoka ndani ya kweli ya NENO LA MUNGU.
Kwa lugha nyingine, mtu mwenye ufahamu sahihi, anayo KWELI ndani yake kwa namna ambayo anapata msaada wa kiMungu katika shughuli zake za kila siku.
UFAHAMU ni TAARIFA zinazoingia na kutoka kila sekunde ndani yangu.
UFAHAMU ni yale yote au jumla ya mambo yote ninayoyajua yaliyo ndani yangu
Ufahamu ni mkusanyiko wa MAARIFA yote ambayo yako ndani ya mtu. Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa na kumcha BWANA ni ufahamu.
Ufahamu ndio MPAKA wa maamuzi na matendo yako kila siku.
Chochote kilichoka ndani ya UFAHAMU wako kitakuwa na faida au hasara kwako na hata kwa watu wanaokuzunguka.
Ufahamu ndio uliobeba tafisiri ya giza na nuru.

Neno letu kuu hili hapa
Mithali 9:10..
Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima;
Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu.

So ufahamu ni kumjua Mtakatifu
Kumjua Mtakatifu...soma Yohana 17:3
Yohana 17:3
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.

So kumjua Mungu ni uzima wa milele na pia ndio ufahamu.
That means mtu yoyote mwenye UFAHAMU lazima ATAKUWA anajumjua Mtakatifu. Kama hamjui Mtakatifu hana UFAHAMU, Au ana UFAHAMU ulioharibika.

So hii inamaanisha kuwa mtu ASIPOMJUA MUNGU anakosa UFAHAMU na kwasababu hiyo anakuwa GIZANI yaani katika UJINGA.
Lakini mtu anapo MJUA MUNGU anapata UFAHAMU na kwasababu hiyo anakuwa NURUNI yaani katika maarifa na kujua.
Kwamba mtu asiyemjua Mungu yupo GIZANI na giza dawa yake ni NURU ndo maana maombi sio tiba ya kila kitu...maombi hayaondoi UJINGA-GIZA....kinachoondoa ujinga ni NURU-UFAHAMU –MAARIFA

Kumjua Mungu ni maamuzi binafsi.
Hapa kwenye kumjua ndo nataka tupachimbe kidogo...
KUMJUA
TO KNOW THE KNOWLEDGE OF THE GOD.
Efeso 1:17
17 Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye;

Kumjua Mtakatifu au Mungu kunakoleta UFAHAMU na UZIMA WA MILELE inahitajika roho ya hekima na ufunuo.

Kumjua Mtakatifu na kuzidi kukua katika UFAHAMU wa kiMungu na hata kukomaa kiimani pia inahitajika roho ya hekima na ufunuo

Itaendelea.....

Ushirika na Mungu!

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.