NGUVU YA UFAHAMU SAHIHI-2
....Inaendelea
Swali: HUKU KUMJUA MUNGU HASA NDO NINI? UKISEMA UNAMJUA MUNGU
UNAMAANISHA NINI HASWA???
Quote
of Raphael JL: Face today with the CONFIDENCE rooted, established and grounded
in trusting the name of the Lord. Repeat after me, I FACE THIS DAY IN THE NAME
OF JESUS AND MY VICTORY IS PREDICTABLE.
Ushirika
na Mungu!
Quote
of Raphael JL: THOSE who TRUST in the Lord are like Mount Zion, they shall NOT
AND NEVER BE MOVED OR SHAKEN but stays forever. May God give you the grace to
TRUST HIM TODAY. You just trust,HE DO THE REST. Join the THOSE Club today.
Ushirika
na Mungu!
Ukiri
Wangu:God is my STABILITY. If am stable
it's because He backs me up always.
Jesus Up!
So tumeona ufahamu ni kumjua
Mtakatifu.
Ufahamu sahihi ni kama nuru gizani.
Tupige hatua moja mbele....
Efeso 1:18
18 macho ya mioyo yenu yatiwe nuru,
mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake
katika watakatifu jinsi ulivyo;
MACHO YA MOYO-Hii ni lugha ile ile
ya neno UFAHAMU WENU UFUNGULIWE ( Luka 24:45) ili muweze KUELEWA
maandiko. Au Zaburi 119:18.
Macho ya moyo ni ufahamu wa ndani
ambao hupokea taarifa za ndani. Hili eneo la ufahamu ndio macho ya mtu
yanayomsaidia kutfisri mambo ya ndani.
GIZA-UJINGA
NURU-UFAHAMU
WA KWELI YA MUNGU
Hivyo mtu asiye na UFAHAMU WA KWELI
YA MUNGU-yuko GIZANI.
Huwezi kulielewa neno la ufalme wa
mungu bila roho ya ufunuo.
You cant have knowledge about god
without revelation.
But knowledge is a function of
wisdom. Ni hatari kuwa na ufahamu bila hekima
Ukijua mambo mengi na hujui namna ya
kuyatumia utakuwa mtumwa mwenye mali zote.
Unaweza ukawa na silaha kali zaidi
ila kama huna hekima unaweza ukapigwa na silaha yako.
Kuna watu wameokoka lakini wanaishi
kama watumwa.
Kwasababu aidha hawana ufahamu wa
kutumia wanachojua au wana ufahamu wa uongo.
Unaweza ukawa mtoto wa mfalme
lakini unaishi kama mtumwa au chokoraa
Wapo walokole wengi sana
wanaotamani maisha ya wasiookoka, wanatamani mali zao, mavazi yao, nyimbo zao
na maisha yao kwa ujumla....as IF wao hawana kizuri hata kimoja.
Wana wa NURU wanatamani nyimbo za
wana wa GIZA, wanatamani mavazi yao, wanatamani make up zao, wanatamani vitu
vyao...hii ni ishara kwamba huenda hawajui WALIVYONAVYO au ni ujinga wa ujumla.
Mfano: Unamkumbuka Mwana Mpotevu?
Baba yake alikuwa TAJIRI wa kutupwa...ila kwa mapenzi ya ujinga wake aliishi na
nguruwe mpaka akili zilipomrudia....
MACHO YA MOYO wako yakitiwa NURU
maana yake ufahamu wako unapofunguliwa kwa kumulikiwa mwanga wa Neno la Mungu
kuna mambo unaanza kuyaelewa ambayo hujayaelewa miaka na miaka. Ghafla unaanza
kuona vitu vinaeleweka na unaanza kujiona ulivyokuwa mjinga...kwasababu UFAHAMU
WAKO UMETOLEWA GIZANI na kuletwa NURUNI..
Yohana 1:4-5
inasemaje?
4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima,
nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.
5 Nayo nuru yang?aa gizani, wala
giza halikuiweza.
Kumbe...nuru ina nguvu kuliko
giza.....ufahamu wa neno la Mungu una nguvu kuliko ujinga..
Ipo kanuni kwenye Yohana
8:31-32
31 Basi Yesu akawaambia wale
Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli
kweli;
32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo
kweli itawaweka huru.
Darkness is not the opposite of
light-giza sio kinyume cha nuru. Giza ni kutokuwepo kwa nuru. Pasipo na nuru
pana giza. So kuna gharama ya kulipa ili kukaa ndani ya neno la Mungu-kulisoma,
kujifunza, kulitafakari, kuliomba, kurikiri, kuliwaza na kuliruhusu liongoze
mwenendo wetu kila siku.
Maana yake ni hivi.....kanuni ya
kitu kuwa kinyume ya kingine ni kwamba hivo vitu vinaweza kuishi pamoja, they
can co-exist. So nuru na giza haviwezi kukaa pamoja kwa wakati mmoja...so giza
sio kinyume cha nuru bali ni kutokuwepo kwa nuru...mahali popote nuru
isipokuwepo giza hutawala....giza ni ujinga au dhambi...nuru ni ufahamu wa kiMungu
Bwana Yesu anasema....kaeni katika
neno langu...maana yake live in, live through, live for....yaani ishi ndani
yake, ishi pamoja nae...maana yake neno lake ndio liwe kamusi inayokupa maneno
na misamiati ya kutumia kila siku....maisha yako yote ya kila siku yawe neno la
Mungu....neno la Kristo na lijae na likae kwa wingi katika hekima
yote....moyoni mwangu nimeliweka neno lako nisije nikakutenda dhambi.
Hapo sasa ndo tunaenda kwenye Mathayo
5:14-wewe ni nuru kwao-matendo yako, maneno yako na mwenendo kwa ujumla
unatakiwa uwape nuru yaani uwape kuona namna wanavyoenenda kwa kuangalia maisha
yako...unavyowajibu, wanaona majibu yako yana hekima ndani yake kwani wewe ni
nuru yaani wewe una kweli ya mungu ndani yako inayoathiri mpaka watu
wanaokuzunguka....Bwana Yesu akasema watu hawawashi taa na kuziweka chini ya
pishi bali juu ya kiango ili ionekane na wote...pia inamaanisha hata kama
unakaa na hao watu na wako gizani inamaanisha ni wajinga, wewe kwakuwa una nuru
hutendi wanavyotenda wao kwani wewe ni mwana wa mchana, mwana wa nuru na
matendo yako ni ya nuru na sio giza.
Matayo:5.14
Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji
hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima.
Maana yake nyie mnayo maarifa na
ufahamu wa kiMungu ambao ulimwengu unauhitaji sana.
Kuna mambo matatu makubwa ambayo
mtu yoyote ambaye MACHO YA MOYO WAKE yametiwa nuru huwa anayaona na kubadilika
kabisaaaaaaaaaaaaaa......
Itaendelea...
Hakuna maoni: