NGUVU YA UFAHAMU SAHIHI-3
...Inaendelea
MAMBO
MAKUBWA MATATU YANAYOKUJA MACHO YA MOYO WA MTU YANAPOTIWA NURU
Waefeso:1.18
macho ya mioyo yenu yatiwe nuru,
mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake
katika watakatifu jinsi ulivyo;
1.
TUMAINI LA MWITO WAKE-Kwamba lipo TUMAINI LA WITO au KUITWA
au MWITO ambalo mtu hulijua akishatiwa NURU ndani ya ufahamu wake. Kila mtu aliyeokoka anatakiwa kuwa na kujua
kuwa tumeitwa kwa tumaini linaitwa BLESSED HOPE....kwamba si tu katika wakati
huu wa sasa bali zaidi sana katika wakati waa umilele ujao...hatuchoki kwani
tunajua tumeitwa na aliyetuita ni Mungu....kila aliyeitwa anajua lipo kusudi la
kuitwa kwake....anaishi akiwa amejaa SHAUKU akijua kuwa mwisho wa siku upo utukufu
mkubwa zaidi ya mateso tunayopitia leo.
Mfano:
Ni kama leo upokee simu kuwa unaitwa na rais na unatakiwa kusafiri
kesho....haha hahaha wengine hawatalala, utaahirisha kila kitu ili ULE WITO uwe
na thamani kwako....hutakubali kikwazo chochote kiingilie kati WITO huo....ndio
biblia inasema hapa duniani sisi ni wapitaji,wenyeji wetu uko mbinguni....tumeitwa
jamani....
Lazima. Mateso ya imani yako kwake....Warumi
5:3
Blessed Hope!
2 Wakorintho 4:16-17
16 Kwa hiyo hatulegei; bali
ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya
siku kwa siku.
17 Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo
ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana;
2.
UTAJIRI WA UTUKUFU WA URITHI-Macho ya moyo yakitiwa
nuru ni lazima ujue kuwa kwanza WEWE NI URITHI KWA MUNGU na pili ujue kwamba
MUNGU ANAO URITHI KWA AJILI YA WATATKATIFU au watoto wake...mahali pengine
biblia inasema SISI NI WARITHI PAMOJA NA KRISTO...hii inakupa picha kwamba
upande uliopo sio masikini....vipo vitu vya kurithi...tena urithi wa
milele...ila kabla hatujarithi mwishoni tunatumia sasa vile ambavyo Baba yetu
wa mbinguni ametupa. Sisi ni matajiri, sisi ni wakwasi....sio tu wa mali za
mwilini bali zaidi sana wa siri za ufalme wa Mungu.
Jambo la tatu linapatikana msitari
wa 19....ulete hapa
Ukisoma vizuri NENO LA MUNGU
utagundua kuwa mambo mengi tunajitakia wenyewe kwa ujinga na ulimbukeni
wetu....
Hakika Utajiri ni haki yetu tatizo
ni upofu wa rohoni tu.
Waefeso 1:3
3 Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana
wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa
roho, ndani yake Kristo;
Waefeso 1 :6
6 Na usifiwe utukufu wa neema yake,
ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa.
Waefeso:1.19
na ubora wa ukuu wa uweza wake
ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza
wake;
3.
UBORA WA UKUU WA UWEZA-Hapa unaona kabisa kuwa UKUU WA
MUNGU ni wa kiwango cha mwisho na cha juu kabisa kwa ubora...na huu uweza wake unafanya
kazi ndani yetu tuaminio kwa kadri ya utendaji wa nguvu zake. Kumbuka hapa
inaonyesha wazi kuwa nguvu za Mungu zinafanya kazi ndani yetu...Angalia Efeso
3:20 uunganishe hapa....kizuri na cha kufurahisha na kutia moyo ni
kwamba hizi nguvu ndo zile zile zilizomfufua Yesu Kristo toka kwa wafu....wow
wow
Waefeso:3.20
Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya
mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu
itendayo kazi ndani yetu;
Nguvu za Mungu zinafanya kazi
kwenye maisha yetu kwa kutegemea namna ambavyo hizo nguvu ziko hai ndani yetu. Kama
una nguvu za Mungu kiwango cha kijiko huwezi kupata matokea ya maombi kiwango
cha pipa hata kama umeomba masaa mia nane tisini.
So mpaka hapo umeona hayo mambo
matatu makubwa?????????????
Ufahamu sahihi una nguvu sana.
Tumalizie leo na Warumi
1:28 na Hosea 4:6....twende
Warumi:1.28
Na kama walivyokataa kuwa na Mungu
katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye
yasiyowapasa.
Hosea:4.6
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa
maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe
kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami
nitawasahau watoto wako.
Ukisoma Warumi 1:28 na Hosea 4:6
unajifunza nini?
Soma kwa makini mistari yote.
Heri wenye njaa na kiu ya haki.
Mungu hawezi kumtumia mtu ambae
ufahamu wake umejaa mambo ya dunia hii. Ndio maana kila anaeitwa na Mungu
hubadilishwa ufahamu wake ili ufanane na wa yule anaemuita.
What changes first is what you know
about God (your mind), not what you do.
MUNGU AKUBARIKI
Jesus up!
Raphael JL.
Hakuna maoni: