SHIRIKI
SOMO: SHIRIKI
By Raphael JL
Niseme hivi....
Hii nukuu hapa....
Quotes
by Raphael JL:Shiriki mambo ya watu na watu watashiriki mambo yako. Kuwa sehemu
ya timu au kundi halafu hufanyi mambo yaliyomo ni sawa na kutengeneza mazingira
ya kuwalaumu wengine kwa ubora wa ujinga wako. TRANSFORMATION IS ENGAGEMENT.
Mungu
Kwanza-YKM!
Nataka niseme kuhusu jambo hilo
maana linanipigisha kwata moyoni
Kwanza naamini Transformation is a
function of TOTAL ENGAGEMENT....
Niwahamasishe wapendwa watu wakuu
MAISHA NI WATU. MAISHA NI MUNGU. Ukiwa
na WATU WENYE MUNGU wanakuzunguka ujue umeshinda sana. KUSHIRIKI ni zaidi ya
KUWEPO. Kushiriki ni zaidi ya kutoa fedha. Kushiriki ni hata kutoa taarifa
unayodhani inawafaa wengine.
Hivi ninyi hamjaona kuwa kuna
matukio ya maisha ya baadhi ya watu HUCHUKULIWA KWA NGUVU ZAIDI kuliko wengine?
Hamjaona? Na wengi bado hamjaoa, Hamjaolewa, mtaihitaji watu kwenye maisha yenu
itakapofikia matukio hayo.
Najua mna watu wengi maana mko
kwenye magroup zaidi ya 666. So inawezekana group la YKM lisiwe na nguvu na
thamani saaana...ila inaleta gap moja kubwa sana...
Kuna watu toka uchumba wao watu
wameshiriki mpaka ndoa, Kuna watu inasikika juu kwa juu tu, Na wote wako humu
humu. Kuna watu wanafiwa kimya kimya. Kuna watu hata akiumwa mafua tunajua
YOU
CAN’T BE TRANSFORMED WITHOUT ENGAGEMENT...
Kuna watu hawajaona umuhimu wa
kukutana pamoja physically. So hawamaanishi sana hata mkikubaliana kukutana
hawajali sana. Ila kesho na keshokutwa watalalamika kuwa NO BODY CARES...bila
kujua kuwa inaanzia kwao.
NI KWELI MUNGU ANAANGALIA MOYO, ILA
SISI NI WATU, SO TUNAANGALIA MWILI.
Kama upo kwa group au timu na
umekubali kuwepo kwa hiari yako... KUTOSHIRIKI MAKUBALIANO YA TIMU ni UASI.
Ukiwa na mchumba asiefanya
mnayokubaliana? Ukiwa na mpenzi anaekutia moyo kwa maneno na sio matendo? Jikague
kuanzie kwenye FAMILIA YAKO. Nenda kazini kwako. Nenda kanisani kwako. Utaona
hii kanuni...WATU WANAOKUMBUKWA POPOTE
WALIFANYA KITU...walishiriki
Moja kati ya kanuni ya THE VALUE OF
YOUR IDENTITY tulijifunza camp inasema hivi..... YOUR PHYSICAL PRESENCE HAS NO
SUBSTITUTE.....
Mara nyingi huwa nakuja humu na
kusema hili na lile...because I know my presence matters
"YKM Dar ndo group ambalo
nakuja mara nyingi zaidi kuliko any other group...ni kwasababu MKO ACTIVE
sana.....na mna ushirikiano ila bado kuna watu wa kuwasaidia pia...walio
kimya"
Haijulikani bado wako au hawako
kitambo. Haijulikani wanaamni tunachokifanya au hawaamini. HAIJULIKANI tuuuu.
Kuna wengine wakiombwa kuwa viongozi wanakataa...haha hahahah
SASA UTAJUAJE BILA KUFANYA?
UTAFANYAJE BILA KUANZA? UTAANZAJE BILA KUWEPO NA CHA KUFANYA?
Najua humu wamo watu tofauti
tofauti...wakubwa kwa wadogo...waliooa na kuolewa na ambao bado...so kila kundi
linatakiwa lijue namna ya kumchukulia mwingine
Maana hata mimi mwenyewe nikisema
nijihesabie haki kwa STATUS QUO ni vigumu kuwepo humu na kupiga story na watu
tunaofanana tu kuvuta oxygen labda....So wakati mwingine wale waliooa na
kuolewa...yaani toka walivyooolewa au kuoa hahaha haha ndo ikawa mwisho...khaaaaa
MUNGU ANWAONA.
Kuna watu wamo humu hawana
ajira...ila kuna watu wamo humu wana maconnection na wenye ajira...ila sema ndo
vile sasa...NO ENGAGEMENT....
Kuna watu hawajaona umuhimu wa kuja
camp...kuna watu hawawezi kukosa camp...kuna watu wanatamani kuja camp...wote
wamo humu...camp haijalishi umeoa au umeolewa...in fact UKISHIKILIA STATUS QUO
camp inaweza kukusumbua sana maana utaona aaah mambo ya vijana hayo...ila ukija
unagundua khaaaaa mweeee
Katika kufuatilia jambo hili
nikagundua pia ipo ishu ya KIPAUMBELE/PRIORITY...like YKM ni kipaumbele cha
ngapi katika huduma ulizonazo au katika makundi ulonayo...HILI NI JAMBO
BINAFSI...
Basi watu wa Mungu,nikajisemea tu
kuwa niwatie moyo kwa tumaneno hutu tuchache...
SHIRIKI. ENGAGE.
Sio kila siku wewe utapokea tu.
Kuna siku unaamua kutoa hata kama ni kwa kujitoa ufahamu.
WENEED EACH OTHER.
USHIRIKI UNALETA UMILIKI.
Ndo maana kila mtu akitokaga camp
anakuwaga na moto mbaya...wengine moto huzimika baada ya wiki moja na wengine
mpaka leo wamesimama.Lazima kuwe na siri. SHIRIKI. Kumbuka kushiriki kuna
gharama yake. Ukiikimbia gharama ujue umekimbia kuwa matokeo ya mchakato wake.
NI HAYO TU.
MUNGU
AWABARIKI
YKM
FICHUKA
MUNGU
KWANZA
JESUS
UP
Hakuna maoni: