Ads Top

ADUI WA KUDUMU NI SHETANI TU, HATA AKIWA NDANI YA MTU.



ADUI WA KUDUMU NI SHETANI TU, HATA AKIWA NDANI YA MTU

Usije ukategemea kwamba kuna siku shetani atakuja kupatana na Mungu au Mungu kumsamehe kwa ujinga wake alioufanya. Hii ndo maana wana wa Mungu na wana wa shetani hawawezi kupatana kwani wako kwenye falme mbili tofauti na wanawatumikia mabwana tofauti. ADUI WA KUDUMU NI SHETANI TU. Hii ni muhimu ukaielewa ili uache kupambana na watu ukadhani ndio maadui zako. Ukielewa hii utajua kwanini Bwana Yesu alimwambia na kumkemea shetani aliyekuwa ndani ya Petro. SHETANI MBAYA SANA.

Unakumbuka ni akina nani walikuwa marafiki sana, urafiki wao ukaja kugeuka kuwa uadui mkubwa sana? Au unakumbuka watu waliokuwa maadui wakubwa sana ila baadae wakaja kuwa marafiki wa kutupwa? Hii ndio sababu watu husema usiingilie ugomvi wa mke na mume maana kesho watakushangaa sana kuingilia mambo ya watu wanaolala chumba kimoja. Hii ndio sababu kwanini ni vigumu sana kuwa na mwanadamu unaesema kuwa ni adui wa kudumu kwenye maisha yako kwani mazingira na zigezo zikibadilika wakati wowote maamuzi hubadilika. AMINI USIAMINI.

Je, wote waliokuwa adui zako miaka mitano ilopita bado ni maadui mpaka leo? Je, wale waliokuwa marafiki zako wa damu miaka michache ilopita bado ni marafiki zako wa damu leo? Mambo hutokea na watu hubadilika kila kukicha. Ndo maana Mungu mwenyewe anasema AMELAANIWA MTU YULE AMTEGEMEA WANADAMU, AMFANYAE MWANADAMU KUWA KINGA YAKE NA HUKU MOYONI MWAKE AMEMWACHA MUNGU. Hii ni kutokana na ukweli kuwa wanadamu hawategemeki milele. Tuna pwaya sana. ADUI WA KUDUMU NI SHETANI TU.

Ukilijua hili basi unatulia na kuendelea kumwamini Mungu juu ya wanasamu wote kila siku kwani YESU NDIYE RAFIKI MWEMA NA WA KWELI. Huu ni ukweli usiopingika.

By Raphael JL:

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.