Ads Top

USIIFATISHE NAMNA YA DUNIA HII....ADUI WA KUDUMU NI SHETANI TU



17.12.2017
USIIFUATISHE NAMNA YA DUNIA HII, ADUI WA KUDUMU NI SHETANI TU.

Ukiona unatumia muda mwingi kufanya mazoezi ya uimbaji kuliko kusoma NENO LA MUNGU au unatumia muda mwingi kupiga mziki zaidi ya muda unaotumia kuomba na kumtafuta Mungu. Ujue mziki au uimbaji una nguvu kubwa ndani yako kuliko Mungu. Na huenda unaabudu muziki na sio Mungu. Dunia ina muziki wake na Ufalme wa Mungu una muziki wake. Kuifuatisha namna ya dunia hii maana yake ipo namna ya dunia na ipo namna ya Ufalme wa Mungu. Warumi 12:2

Petro alionekana hata kutembea kwake na kuongea kwake kunafanana na Bwana Yesu, sembuse mavazi? Sembuse muziki? Sembuse maneno? Sembuse urembo? Dunia hii ina namna yake ya kufanya kila kitu na sisi tumehimizwa kutokuishi kwa kufuaata namna hii ya dunia. Kanisa likifana na dunia ni hatari sana. Hata kama ni kwa kigezo cha kusema tunataka kuwavuta wa duniani waje kanisani. Huu ni upuuzi. Ni upuuzi kutumia njia za dunia kuwavuta wa duniani waje kwa Yesu. Wizi ni wizi tu hata kama umeiba biblia.

Ni rahisi hata kuanza kubadilisha maneno, ili mradi tu ifanane na kanisa ingawa sio ya kanisa. Sebene la YESU, disko la Yesu, Gospel Flava, Gospel model, Gospel Hip Po, Gospel Singeli, Gospel Jesus etc. Hii ni mifano tu ya maneno ambayo yanatumika kuvifanya vitu vya duniani vikubalike kanisani kwa kigezo cha kuwavuta watu wasiomkubali mungu wamkubali. Utofauti wa chumvi na sukari ni nini sasa kama chumvi imeamua kuwa sukari? Je, hii ni kweli kuwa nuru na giza ni vitu vilivyo tofauti na sio kwamba giza ni utokuwepo kwa nuru?

Je, ni kweli tunaipenda dunia kuliko Mungu anavyowapenda kwa kiwango ambacho tuko tayari kujifananisha na dunia ili tuwapate wa dunia? Utofauti wetu ni nini sasa? ANYWAY.


Raphael JL:

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.