Ads Top

UTAMBULISHO WETU NI UPI JAMANI???



20.12.2017

Kwenye eneo la kuiga tuna vyeti. Tunaiga kila kitu chao na kukipa jina la kiMungu au kuongeza vimaneno vya YESU mbele au nyuma. Tunaiga mpaka ufahamu wetu unaturudia. Tukiona watu wanatusema na sisi tunawaambia SHETANI ALIIBA HIVI VITU NA SASA TUNAVIRUDISHA. Tuko vizuri kweny ehili eneo kwa kiwango ambacho mtu akigusa tu hatumualiki tena kuja kufundisha kwetu maana anatuboa. Tunaiga mengi wayafanyayo.

Tunaiga muziki wao, tunaiga nyimbo zao na kubadilisha maneno tu, tunaiga mpaka wao wenyewe wanajiona wanaiga kwetu. Tunasikiliza nyimbo zao ili tupate vionjo vya kuweka kwenye nyimbo zetu. Hata mtu mzoefu wa muziki akisikia anajua kabisa hapa mwanzo mwa wimbo huu ni EXTRA MUSIKA, pale katikati ni PEPE KALE ila sema maneno ni ya YESU. Hakika, YESU BAKI NA MANENO,MENGINE TUACHIE.

Tunaiga wanavyovyaa na kujipa moyo kwamba MUNGU HAANGALII MWILI BALI MOYO. Tunasahau kuwa MUNGU SIO RAPHAEL. Raphael ana macho yanayoangalia mwili, ila tunajipa moyo kwamba Raphael atakuwa ana shida binafsi kwani anaweza kufuba macho. Tunaiga wanavyovaa mpaka tunavaa chupi madhabahuni na kusema ni KIMINI CHA YESU. Tunaiga sana. Tunaiga namna wanavyochukua video zao na closeup zao, ni sawa kuwasogezea watu makalio ili TUONE UUMBAJI WA MUNGU YEHOVA.

Wakianza wao kufanya lazima na sisi tutafuata hata kama ni kwa kubadilsiha vimaneno vya hapa na pale. Wakishindana na sisi tunashinda. Wakianza kuongea Kiswahili kama kingereza kama watu wanaoumwa meno na sisi tutafuata. Lazima uimbe kama wanavyoimba ili muziki wako uwe na soko ama sivyo utatembeza CD zako kwa bajaj. SOKO LIMEAMUA. Biashara inalipa sokoni sio milimani. Hata hivyo, sio lazima kumsemasema au kumtajataja Yesu kwenye nyimbo au chochote unachofanya kwani kuna watu watakwazika na hivo utapoteza SOKO.

Inawezekana kujifunza kwa asiye amini mambo mengi tu lakini SIO KUAMBATANA NAE maana HAZINA HUKAA MOYONI. Najiuliza, hivi mtu akisikia maneno yangu au lugha yangu mahali ambapo hakuna mtu anaenijua atasema na mimi ni rafiki wa MGALILAYA AU PILATO? Utofauti wetu uko wapi? Ni lazima wao wafanye ili mimi ndo nipate au nijue cha kufanya? Wao wanaiga nini kwetu? Oooh sawa, wanachukua vipaji vyetu na kuvipa hela, wala haina shida. Wanatulazimisha tuimbe nyimbo zao na kuzipiga kwani tunalipwa. Waliokomaa kiroho wanasema UNAWEZA UKASIKILIZA NA KUCHEZA NA KUIMBA NA KUPIGA NYIMBO ZAO NA BADO MOYO WAKO UKAWA BADO UKO KWENYE GOSPEL SONGS.

Kizazi chetu kitafika wapi? Maana mambo mengi yanaanzishwa na wao na kisha sisi tunafanya makaratee na kuyapa majina ya kiYesuYesu na tunfanya. NIA YETU NI NINI? KUSUDIO LETU NI NINI? Mwizi ni nani kwani? MWIZI NI MWIZI TU HATA AKIIBA BIBLIA. Inabidi tufanane nao ili tuwavute kwetu, ila tunaonywa sana: Warumi 12:2, BASI MSIIFUATISHE NAMAN YA DUNIA HII…au hii dunia sio ile iliyozungumziwa?


By Raphael JL:
0767033300

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.