Ads Top

KUMSIFU BWANA KUNAACHILIA KIBALI CHA KUFUNDISHWA NAE


12.01.2018

Zaburi 119:12 “Ee BWANA, umehimidiwa, unifundishe amri zako?
Hili ni kama ombi. Hili ni ombi, tunaona Daud anamuomba Mungu amfundishe amri zake na kumoa sifa. Hakika Daud alikuwa na moyo wa ajabu na ahimidiwe Mungu aliyemfunulia siri hizi za ajabu. Pamoja na hali zote alizopitia na yote aliyokutana nayo, moyo wa Daud hakumwacha Mungu wala hakuacha kumpa Mungu haki yake anayostahili kama Mungu. Hii ni kwasababu hakuna kinachombadilisha Mungu, yaani Mungu habadiliki wala habadilishwi na hali zetu au tunayopitia. Yesu Kristo ni yeye yule, jana, leo n ahata milele. Tunaona Daud akimsifu Mungu kwa moyo wa dhati kabisa, akisema ee Bwana uhimidiwe.

Watu wengi tumekuwa tunamsifu Mungu kwa kutegemea majira tunayopitia na kujikuta kuwa tunapopita katik vipindi vigumu kwenye maisha tunapoteza moyo uliochangamka unaotakwa kumpa sifa Bwana. Ni vema tukajua kuwa kumsifu Bwna kunaachilia kibali cha kufundishwa nae, yaani Mungu akipokea na kukubali sifa kutoka kwetu ni rahisi sana kutufundisha pale tunapomuomba kwani sifa zinaufungua moyo wake kwetu. Hii inamaanisha kuwa ni lazima tuwe na ufahamu sahihi na mzuri kuhusu Mungu, yaani tumjue Mungu vizuri. Kumjua Mungu ndio kitu peke ambacho tunakiona alikuwa nacho Daud katika maisha yake. Alimjua Mungu kwa namna ambayo ilimfanya kuwa mtu wa tofauti sana. Daud na Saul wote walikosea, ila angali namna Mungu aliwachukulia kutokana na moyo wa kila mmoja wao. TUJIFUNZE KUMSIFU BWANA KATIKA HALI ZOTE.

For the King and His Kingdom,
Pastor Raphael JL:
0787110003.
DODOMA.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.