MAUSIA YA MUNGU YANA NJIA YA UZIMA
27.01.2018
Zaburi 119:27 Unifahamishe njia ya mausia yako, Nami nitayatafakari maajabu yako.
Ukisoma kwa tafsiri ya kingereza, huu msitari unasema, nisababishe ili nielewe njia za mausia yako. Ni kama kusema huyu Mzaburi alijua, hata kuelewa njia ya mausia ya Mungu ilibidi Mungu amsaidie aweze kuelewa. Ndo anaomba Mungu amfahamishe njia za musia au njia za neno lake kwani anajua ndani yake kunayo maajabu. Pia tunaona kuwa ipo nguvu ya kutafakari neno la Mungu kwani ndani yake yapo maajabu.
Utaona pia kuwa haya ni maombi ya kuomba msaada wa Mungu kwenye maisha yake, anaomba aaidiwe kuelewa sheria na amri za Mungu. Hii ina maana kuwa hatuwezi kuliewa neno la Mungu, hatuwezi kuzielewa njia za sheria yake bila maada wake. Nasi tunajua kuwa ni Roho Mtakatifu ndiye anaetusaidia hata kuelewa haya. Wakati mwingine ukiwa unasoma biblia n unaona huelewi ni vema ukumbuke kumuomba Roho wa Mungu ili akusaidie kuelewa maana usipoelewa neno haliwezi kukusaidia. Hii inamaan kuwa mausia ya Mungu yana njia ambayo sisi sote tunatakiwa kufundishwa ili tuweze kuyaelewa kwani kadri tunavyotafakari mausia au neno au sheria za Mungu ndivyo tunavyodzidi kuona maajabu yaliyomo ndani yake.
For the King and His Kingdom,
Pastor Raphael JL:
0787110003.
DODOMA.
Hakuna maoni: