Ads Top

MDOMO WAKO KINYWA CHA MUNGU.



13.01.2018

Zaburi 119:13 “Kwa midomo yangu nimezisimulia hukumu zote za kinywa chako?
Kwa midomo yangu nimezisimulia hukumu zote za kinywa chako. Maneno mazito haya. Nawaza kwa midomo yangu huwa nafanya nini? Huwa natamka nini? Huwa naitumiaje midomo yangu? Kubariki au kulaani? Au midomo inafanya uzushi? Kumbe midomo yetu inatakiwa kuzisimulia hukumu za Mungu ambazo zinatoka katika kinywa chake. Maana yake kuitumia midomo yetu kusema haki ya hukumu za Mungu, yaani kuwaambia watu wengine kuhusu hukumu za Mungu. Nasi twajua kuwa hukumu zote za Mungu ni za haki na zina haki ndani yake. Ni vema na wengine wakajua hayo. Ili wajue ni lazima sisi tunaojua tayari hukumu za Mungu tuwasilimulie.

Hili jambo haliwezi tu kutokea bila kuwa na mpango wa makusudi. Ni lazima ujue kabisa, akili zako ziwe timamu kujua kuwa midomo yako inatumika vyema. Vipi viungo vyako vingine vya mwili? Unavitumiaje? Vipi simu zako? Vipi vipaji vyako? Vipi pesa na mwili wako? Kumbe midomo yetu inaweza kutumika kama silaha za haki katika kuzisimulia na kuzitangaza hukumu za Bwana ili hata wale wanaoonewa wajue mahali sahihi pa kukimbilia wakiwa wanahitaji haki.

Kumbuka, lakini kuwa mdomo hauna nguvu kuliko mawazo. Unayowaza utayakiri na kuyasimulia.

For the King and His Kingdom,
Pastor Raphael JL:
0787110003.
DODOMA.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.