Ads Top

MWANACHAMA WA KUDUMU WA UHARIBIFU, MAJUTO NA HASIRA.



08.01.2018

 Zaburi 119:8 "Nitazitii amri zako,Usiniache kabisa."

FAIDA ZA KUMJUA MUNGU
Ndo maana KUMJUA Mungu ni ufunguo wa kwanza kabisa wa mtu kuwa na UTULIVU. Kumjua Mungu kunakupa amani ipitayo mahangaiko yote ya dunia. Kumjua Mungu kunakupa ujasiri wa kuwa huna hela na bado UNATABASAMU. Kumjua Mungu kunakufanya useme BWANA NDIYE MCHUNGAJI WANGU. Daudi alijua kuwa Mungu hawezi kumuonea na wala Mungu hamuonei mtu...Daudi atakuwa alishaona tokea ameanza KUMJUA MUNGU namna ambavyo amehukumu watu na mataifa...Kumbuka Daudi alikuwa haendi kupigana vita bila kumuuliza Mungu kwanza...na kile kibali ndo kilikuwa ushindi wake.Ukisoma biblia utagundua kuwa ni Daudi tu kati ya wafalme wengine ambaye HAKUPOTEZA VITA hata moja na aliwamaliza adui zake wote na ndo maana Solomon  alikuja na kustarehe na kujikusanyia wanawake kwani HAJAWAHI KWENDA VITANI.

       Mungu alitupenda AKATOA.  Sisi tukimpenda TUNATII. KUTOA kwetu ni KUTII.HUWEZI KUMPENDA MUNGU KULIKO UNAVYO MTII.YOU CAN NEVER LOVE GOD MORE THAN YOUR OBEDIENCE TO HIM.

Daudi aliweka KIAPO, aliazimu moyoni mwake, aliweka MSIMAMO WENYE NIDHAMU, alikuwa tayari kulipa gharama ya KUZITII AMRI ZA BWANA maana pia alijua akifanya hivyo Mungu hawezi kumuacha. Alimjua Mungu to that level. Tukimtii Mungu, hawezi kutuacha hakika.

KUZITII AMRI ZA MUNGU ni pamoja na kufanya na kutekeleza yote yatokanayo na yaambatanayo na amri hizo. Ni moja kati ya maamuzi magumu ambayo MWANAFUNZI WA YESU anatakiwa kuyafanya. Ni amri ya Mungu kwamba sisi tunatakiwa KUOMBA...je tunaomba? TUNATII? au tunachat na kuangalia tamthilia zaidi kuliko kumtii Mungu? Ni amri kusoma Neno na kutafakari...je tunatii? Ni amri kuutafuta kwanza UFALME wa Mungu na HAKI yake...je tunautafuta? HUWEZI KUTAFUTA AMBACHO HUJAPOTEZA.

Ni AMRI kusamehe, je tunasamehe? Ni amri kusaidia masikini, je tunafanya hivyo? TUNATII? Utii haupimwi kwenye vitu tunavyovichukia, no. UTII NI GHARAMA. UTII NI KUACHA VILE UNAVYOPENDA,ili uyapishe mapenzi ya Mungu kwenye eneo husika. BWANA YESU ALITII MPAKA KUFA. Sisi tunaacha mangapi ya dunia kwa ajili ya Mungu wetu? Tukikatazwa kuvaa vimini tunajitetea, tukikatazwa KUIFUATISHA NAMNA YA DUNIA hii kwa staili za maisha yao kama muziki wao, fasheni zao, lugha zao tunajitetea kuwa WOKOVU SIO MGUMU KIHIVYO. WOKOVU ungekuwa rahisi kihivyo. BWANA YESU hakuwa na haja ya kufa. Alikufa ili atupe wokovu, HOW CAN WE LIVE LIKE HIS DEATH WAS NOTHING?

“ UKIONA UNAMTII MUNGU HUKU UNATABASAMU UJUE UNAJITII MWENYEWE”
 Ilimghalimu Bwana Yesu MAUTI ili AMTII MUNGU. Mauti ndio gharama ya juu na ya mwisho ya UTII. Sembuse unashindwa KUOMBA kisa umetoka kazini umechoka? Ila ukiwa na uchovu huo wa kuomba au kusoma neno unaweza kuchat au kuangalia tahmthilia mpaka saa saba usiku.

 Tutapataje KUPONA tusipoujali wokovu MKUU NAMNA HII? Wokovu uliomfanya Yesu afe msalabani. Alitamani kukikwepa kikombe cha wokovu ila alikubali mapenzi ya Mungu yatimie. Haiwezekani ukamtii Mungu kirahisi rahisi tu, huku unaendelea na KUIGA NAMNA YA DUNIA HII, huku unaendelea KUWA SUKARI YA DUNIA badala ya chumvi. UTII NI GHARAMA. Huwezi kugharamia kama kitu HAKINA THAMANI. Kama kuna eneo unamtii Mungu basi angalia ni gharama gani unaingia kutii hicho cha Mungu.

KUMTII MUNGU ni kutii mawazo yake, kutii amri zake, kutii jina lake, kutii sheria zake, kutii watumishi wake, kutii nyumba yake, kutii neno linalotoka kinywani mwake na ni kumtii ROHO WAKE. HUWEZI UKATII NUSU NUSU. Unatii kwa ujumla. KUMTII MUNGU NDIO SAWA PEKEE YA KUMALIZA UBINAFSI.

 Majeshi yote duniani yameiga mfumo wa Mungu wa mamlaka. UNATII KWANZA,UTASIKILIZWA BAADAE kama ni lazima. Wafuatilie waliofanikiwa kumtii au wale walioshindwa kumtii Mungu kwenye biblia, walipewa tu maelezo ya nini cha kufanya, mengine watajua baada ya kufanya. Ibrahim aliambiwa atoke aende asikojua ila alipofika mahali sahihi aliambiwa na akaelewa. Musa? Daudi? Isaya?

“UKIAMBIWA NA MUNGU NA UKAAMINI NA KUTHIBITISHA KUWA NI YEYE, WEWE FANYA TU ULIVYOAMBIWA”
Unashuhudiwa muombee mtu fulani, wewe mpaka umuulize huyo mtu...eti nikuombee nini maana nasukumwa kukuombea....ndo maana baada ya kumuuliza tu unajikuta umeanza umbea na story zisizokuhusu kwa kuwa umeacha kazi ulopewa. Tatizo letu TUNAPENDA SANA SIFA NA UMAARUFU hata kama ni wa kuigilizia.

UTII HAUWEZEKANI BILA IMANI, yaani lazima umwamini UNAETAKA KUMTII. Kma huna imani nae na unamtii hiyo tunaita NIDHAMU YA WOGA.

KUMTII MUNGU ni kukubali kuwa huyo Mungu unaemtii ANA MPANGO MZURI na wewe, anakuwazia mema na hayuko tayari kukuona unapotea na ndio maana anakuleta ujumbe ambao unatakiwa kuutii ili ufanikiwe. MAFANIKIO YA KWELI NA KUDUMU NI KUMTII MUNGU. Maana Mungu anajua kitakachotokea kama tutamtii, ni kama huwa anasubiria kuona furaha yake inatimzwa kwa kutii kwetu. Ninaamini, tusipotii huwa tunamuhuzunisha sana Baba Yetu wa Mbinguni. KUNA HASARA NYINGI TUNGEZIEPUKA KAMA TUNGEMTII ROHO MTAKATIFU.

Usipomtii Mungu unafanikiwa kuwa mwanachama wa kudum wa UHARIBIFU, MAJUTO na HASARA. Chaguo bado ni lako wewe.

For the King and His Kingdom,
Pastor Raphael JL:
0787110003
DODOMA

Maoni 1 :

Inaendeshwa na Blogger.