Ads Top

NENO LA MUNGU LINATEGEMEKA LITEGEMEE.



18.06.2017

Jesus Up!
Mithali 30:5
Kila NENO la Mungu limehakikishwa; Yeye ni ngao yao wamwaminio.
Ni kweli kwamba KILA neno la Mungu LIMEHAKIKISHWA, yaani limepimwa na kuthibitishwa kuwa linafaa kwa matumizi yetu kama wanadamu. Maana yake limepitishwa kwenye mchakato wa kulijaribu ili lionekane linafaa kwa kiwango gani na mwisho likaonekana kuwa hakika linafaa. Mimi na wewe tunaweza kulitegemea kwani linategemeka,unaweza kuliamini kwani linaaminika. Basi amua leo kuliamini,yaani kulitii kwa kile linachosema. Kaa mbali na manabii na walimu na wachungaji wa uongo wanaotaka wao ndo wawe neno la Mungu.

Zaburi 12:6
Maneno ya Bwana ni maneno safi, ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi, iliyosafishwa mara saba.
Neno la Mungu linategemeka,litegemee. Linaaminika,liamini na kuliamini ni kulitii kwa kile inachosema. Neno la Bwana ni safi kabisa, maana yae limesafishwa ili kusafisha,yaani WATAKASE KWA ILE KWELI,NENO LAKO NDIO KWELI na pia ukisoma Yohana 15:3 unakutana maneno haya Bwana Yesu akiwaambia wanafunzi wake kwamba ninyi mmekwishakuwa safi kwasababu ya lile NENO nililowaambia. Ni kweli neno la Mungu limesafishwa mara saba Zaidi ya dhahabu inayotakaswa kalibuni na ikitoka thamani yake huwa juu sana, si Zaidi sana kwa neno la Mungu?

Zaburi 19:8
Sharia ya Bwana ni ya adili, huufurahisha moyo. Amri ya Bwana ni safi,huyatia macho nuru.
Ungetamani nini Zaidi ya sharia ya Bwana au neno lake? Mengineyo yote yanapita isipokuwa neno la Bwana Mungu wetu. Kwani neno lake Bwana na sharia zake ziko imara kukushika na kukuimariha na pia zinafurahisha moyo. Amri zake ni safi na huyapa macho nuru,ndiyo ni nuru ile inayoleta uzima kama Yohana 1:4-5 inavyosema ndani yake ndimo ulimokuwemo uzima,nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza. Haleluya. Neno la Bwana huyatia nuru macho yangu hakika, huyapa ufahamu na hasa macho yangu ndani ya moyo wangu kama Efeso 1:18 inaniombea hivi macho ya moyo wangu yatiwe nuru…haleluya. Usisahau Bwana Yesu akisema Mathayo 5:14a inasema ninyi ni nuru ya ulimwengu.

Zaburi 119:140
Neno lako limesafika sana,kwahiyo mtumishi wako analipenda sana.
Ukimpenda mtu utafanya mambo yanayodhihirisha unampenda,utakuwa na muda nae na kulipa gharama ya kumuhudumia. Kama unalipenda neno la Bwana jifunze kuwekeza kwenye hilo maana lina utajiri usio na kifani,yaani kwakuwa ni neno safi basi hata wewe litakusafisha basi lifanye kuwa rafiki yako. Lissome,acha kupitia tu maana hata hawa tunaosema ni wadanganyifu hulitumia neno la Mungu kwa uongo.

Basi sasa, neno hili la Mungu likae na lijae kwa wingi ndani yako katika hekima yote,yaani katika mambo yako yote unayofanya na ujishauri. Ukweli ni kwamba,utaburuzwa sana kama humjui Mungu katika neno lake namba alivyojifunua. Utaishi kama mtumwa na utawaabudu watu na kuwaheshimu kuliko unavyomuheshimu Mungu wako. Ayubu anasema mjue sana Mungu ii uwe na Amani. Na pia tusisahau kuwa neno la Mungu ni kama mvua ishukavyo, na theluji kutoka mbinguni, wala haitarudi huko, bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula, Isaya 55:10. Basi acha neno la Mungu likunyweshe na kukuzalisha na kukuchipuza ili upate chakula na mbegu.

Kwa mafundisho ya neno la Mungu,
By Pastor Raphael JL:
Mungu Kwanza.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.