Ads Top

NITAJIFURAHISHA ILI NISILISAHAU NENO LAKO.



16.01.2018

Zaburi 119:16 “Nitajifurahisha sana kwa amri zako,sitalisahau neno lako.
Furaha ya Bwana ni nguvu ya kila anaemwamini. Kumbe ipo siri hapa ya kujifurahisha sana kwa amri za Bwana ili tusilisahau neno lake. Lazima kuijua hii siri. Nitajifurahisha maana yake kuna  namna naweka bidi tokea ndani yangu, nitakusudia kujifurahisha, kuwa na amani na utulivu unaopatikana ndani ya amri za Mungu. Pia ni wazi kuwa kujifurahisha kunasaidia sana katika kuimarisha kumbukumbu ya kutokusahau maana kitu unachokipenda na unakifurahia sio rahisi kukisahau.

Huwezi kujifurahisha kwenye amri usizozijua. Mpaka ufike kwenye kiwango cha kujifurahisha ni lazima uwe umezipenda sana. Mpaka uwe umezipenda sana ni lazima uwe umezitii na hakika umeona faida yake. Hii sio kazi nyepesi. Kujifurahisha katika amri za Mungu ni lazima kitu fulani kiwe kimefanyika na kutokea ndani yetu ambacho kinatufanya tuone thamani ya kujifurahisha ndani ya neno lake. Hapo kuna mambo mawili makubwa ya kufahamu. Moja ni kuwa na furaha inayozaliwa kwa kuwa na ushirika na neno la Mungu kwani neno lake ndio kipimo cha kumjua. Furaha inakuja kwa kujua. Hata ukipita kwenye magumu, kama tu unajua Mungu yuko pamoja na wewe unaweza kucheka kati kati ya vita. La pili ni kuamua sasa kujifurahisha katika amri zake, hii inahitaji pia kuamua na sio bahati.

For the King and His Kingdom,
Pastor Raphael JL:

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.