Ads Top

SHUHUDA ZA BWANA NI BORA KULIKO MALI MENGI.




14.01.2018
Zaburi 119:14 “Nimeifurahia njia ya shuhuda zako, kama kwamba ni mali mengi?
Daud alifika mahali ambapo kitu pekee kilichokuwa kinampa utoshelevu na kutulia ni Mungu na shuhuda na neno lake. Alimpenda sana Mungu. Ni kama alifika mahali ambapo moyo wake ulimuona Bwana kuwa hatma ya kila hali anayopitia. Huku kumjua Mungu kulimpa Daud furaha ya kweli moyoni mwake. Ni kama vile Daud alifika hatua ya kugundua kuwa shuhuda za Bwana pamoja na njia zake zote ni bora sana kuliko kumiliki mali mengi au mali nyingi.

Ukipiga mahesabu ya mtu mwenye mali, kama mali hizo alizipata kwa haki ni wazi kuwa anatakiwa kuwa mtu mwenye furaha sana maana anao utoshelevu. Huyu mtu ana chakula, ana mavazi ana pesa, ana mali za kutosha. Moyo wake unajaa furaha tu kwasababu anamiliki mali. Kwani wewe haijawahi kukutokea unapokuwa na pesa ambazo unaziona ni nyingi vile unajawa na furaha, unakula bila kuwa na wasiwasi wa kupungukiwa hata unaweza kumpa mwingine ofa? Hiyo furaha sasa ipeleke kwenye kumjua Mungu na shuhuda zake na njia zake. Furaha zaidi kwamba umezijua njia za shuhuda za Bwana.

For the King and His Kingdom,
Pastor Raphael JL:
0787110003.
DODOMA.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.