SIO KILA MIKONO ILIYOINULIWA INAMWINUA ANAESTAHILI, MOYO NDIO UNANYANYUA MIKONO.
17.02.2018
Zaburi 119:48
Na mikono yangu nitayainulia maagizo yako niliyoyapenda, nami nitazitafakari amri zako.
Sasa ninazidi kuelewa sana. Unachokiinulia mikono unakiinua chenyewe lakini pia unamaanisha uko chini yake na kwa kweli unakipenda. Maagizo ya Mungu yapaswa kuinuliwa mikono kama ishara ya kukubali kuwa chini yake lakini pia kama ishara ya kukubali kuwa maagizo ya Mungu yako juu na sisi hatuna nguvu zetu wenyewe bila kuwa chini ya hiyo mamlaka. Pia inamaanisha kwa kuwa maagizo yake tunayapenda na lakini tumeona siri na utajiri unaopatikana ndani ya maagizo yake, hakika tunapaswa kuinua mikono yetu kama ishara ya kuridhishwa na ukuu wa maagizo ya Mungu.
Mtu akikwambia anakunyanyulia mikono unaelewa maana yake nini? Amekukubali. Amekushindwa. Amekuelewa sana. Umemuweza. Hana namna ingine. Hakuwezi. Sasa piga picha kuwa na mtazamo kama huo kuhusu maagizo ya Mungu ndani ya neno lake halafu nyanyua mikono yako. Ila kuna jambo moja la kufahamu katika hili jambo la kunyanyua mikono. kunyanyua mikono na kwenyewe hakutokei tu kwa kuwa na wengine wanafanya hivo au kwa kuwa ni muujiza fulani, hapana. kunyanyua mikono ni mchakato wa mambo au vitu kadhaa. Kwanza lazima uwe na mikono yenyewe ya kunyanyua. Lakini pia.
Lazima ujue kuwa moyo ndio unaonyanyua mikono, mikono haiwezi kunyanyuka yenyewe tu bila maamuzi ya moyo na haya maamuzi yanategemea sana hali na ufahamu wa mtu husika. Yaani kama moyo uko vibaya mikono haiwezi kuinuka hata chembe. Kama una ufahamu mbaya basi na mikono pia itakuwa mibaya kwa kiwango cha moyo. Wewe fikiria kunyanyulia mikono maagizo ya Mungu. Ni lazima uwe na ufahamu na ufunuo sahihi. Ni lazima uelewe na ukubali. Ni lazima tu yaani ufike mahali ukubali tokea ndani kwenda nje. So unaona hapo kuwa kunyanyua mikono ni kukubali kwa kiwango cha juu sana. So kuinua mikono hapo, inamaanisha sana kutamani na kuwa na shauku ya maagizo ya Bwana. Kutaka kuyafikia na kuyapata. Kutaka sana kuyagusa na kuyatafuta.
Lazima kuwe na sababu ya kunyoosha mikono ili mikono itemize kusudi lake. Ila kumbuka tu kuwa moyo ni mkubwa kuliko mikono.
For the King and His Kingdom,
Pastor Raphael JL:
0787110003.
DODOMA.
Hakuna maoni: