Ads Top

KOSA LA BALAAM -HESABU 22:7. - UJIRA WA UGANGA.

6. KOSA LA BALAAM
Kosa la Balaam linapatikana katika kitabu cha Hesabu 22,23 na 24. Hili ni kosa la KUTOKUTII SAUTI YA MUNGU yaani KUTOKUMTII MUNGU. Ni kosa la kukosea kwa kuamua huku ukijua kabisa yaliyokupasa kufanya kwani ulijua nini sahihi cha kufanya. Mungu alimwambia Balaam USIENDE PAMOJA NAO (akina BALAKI) wala USIWALAANI WATU HAWA MAANA WAMESHABARIKIWA. Hi indo ilikuwa sauti ya Mungu kuhusu kazi ambayo Balaki mfalme alitaka Balaam mtu wa Mungu aifanye kwa kuwalaani wana wa Israel kinyume na mapenzi ya Mungu. Ni wazi kuwa Mungu alishamjibu Balaam kuwa hao watu hawawezi kulaaniwa maana wameshabarikiwa na Mungu alimpa Balaam jibu hili mwanzoni kabisa.


UJIRA WA UGANGA UNASUMBUA SANA, Balaam akishakupata ujira wa uganga aliendelea kumshawishi Mungu ili aende na hao watu na kweli ukisoma utaona Mungu anamruhusu kwenda kwa masharti ya kufanya atakachoambiwa. Ni rahisi kusema Mungu alimruhusu lakini tunafahamu kuwa Mungu alimkataza kwenda kuanzia mara ya kwanza na tena akimpa sababu ya msingi kabisa kwanini jambo hio haliwezekani.
Akili za Balaam hata leo zipo na zinafanya kazi, zimezaa kizazi chenye ulemavu wa akili katika kufikiria mambo na utendaji wa Mungu. Hata wewe unaweza ukajikuta unataka miujiza au manufaa ya haraka haraka au uko tayari kuuza moyo wako kwa ajili ya pesa.


Unataka unabii kwa kupanda mbegu, yaani usipotoa mbegu MUNGU ANAPIGA KIMYA ila ukitoa tu maunabii yanakuja kama mvua ya mawe. Watu wamebadilishwa huduma zao, kazi zao, majukumu yao na hata mioyo yao kwa ajili ya UJIRA au malipo ya uharibifu. Ni muhimu kujua kuwa huwezi ukaishinda rushwa kama hujawahi kukutana nayo na usiichukie.
Kwasababu ya pesa watu wamebadilisha jumbe zao. Alipewa ujumbe A, ila baada ya kujua anakoenda kuhubiri ni watu wenye pesa akabadilisha ujumbe kwa NGUVU YA UJIRA WA UGANGA. Ni hatari na vigumu kwa kiwango gani kusimama katika msimamo wa Imani mbele ya pesa?


Ona UJIRA WA UGANGA ulivyobadilisha uvaaji, uimbaji na maisha ya Ukristo kwa ujumla. Kwenye upande wa siasa atakuja kuongelea Yesu mwenyewe atakaporudi mara ya pili tena hivi karibuni.


UJIRA WA UGANGA. Unabii wa kupanga foleni, ni kupokea magari tu na manyumba maana Yesu alikuwa masikini kwa ajili yetu na sasa ni wakati wetu wa KUMILIKI. Ingawa kimsingi umasikini wa rohoni hauondolewi na vitu vya mwili.

"Kama kanisa lako magari hayajapaki nje kwa idadi ya kutosha, basi wewe ujue huna Mungu"....KWELI? Huu ni wendawazimu kumlinganisha Mungu na TOYOTA. Ni kweli kwamba Mungu anaweza kukupa hayo yote lakini kutokuwa nayo hakumfanyi Mungu awe mdogo au asiwe na nguvu. Ni lazima kutoa kipaumbele

Kwa ajili ya UJIRA WA UGANGA watu wameacha kuimba nyimbo za kumwinua Mungu na kuanza kuimba nyimbo za GIGKOKOZ PURE MISSION SANDAKALAWE mfano wa zile nyimbo wanazoimba waganga wa jadi.

NB: KUKARIPIWA,KUONYWA SIO KUHUKUMIWA.


YKM: Satisfied In Jesus, Fulfilled In Christ.

Raphael JL
+255 78710003
Dodoma, Tanzania

Insta: @raphaellyela
Youtube: Raphael JL
Web: www.ykm.or.tz
Www.fichuka.blogspot.com

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.