THAMANI YA NGUVU YA UWEPO WAKO- YKM CAMP MARCH 2018 DODOMA (EFC 2018)
THAMANI YA NGUVU YA UWEPO WAKO
Hakikisha lipo jambo unalifanya, ushiriki wako, kama huna unalofanya uliza, nguvu yauwepo wako ni ushiriki.
Jifunze kushirikiana na watu wasiofanana na wewe lakini mlio na lengo moja.
Hakikisha unazo taarifa sahihi za mahali ulipo na uzifanyie kazi ipasavyo.
Fahamu wajibu wako kwa kila nafasi uliyopo.
Nafasi yako popote haiwezi kuchukuliwa na mtu mwingine yoyote isipokuwa wewe pekee.
Usichojua uliza, unachojua fundisha, unachoweza fanya.
Moyo una nguvu kuliko mikono, wekeza katika kuwa na mahusiano mazuri na kila mtu ili
uweze kufanya nae kazi.
Amua kugawa majukumu kama unaona hauna stamina ya kujigawa mahali tofauti ili
ufanye kwa ufanisi na ubora bila kujitetea.
Wasiliana na wanaokuhusu kadri unavyoweza na uhakikishe unakuwa mtu mzuri kwa
kuwafanya wengine wawasiliane na wewe.
Wazo lolote la uovu linapoingia ni lazima utubu instantly maana ukiacha linatengeneza
kitu (bomu).
Usidhrau jambo lolote unaloliona dogo, maana ukubwa wa kitu umefichwa ndani ya udogo
wake kama utaweza kuona.
Unavyojiona ndivyo wengine watakuona. Fahamu kuwa wewe ni wa tofauti na wengine
unaofanya nao kazi walivyo.
NGUVU YA KUKUTANA PAMOJA
Unavunja mipaka ya kimazingira, unapokutana na watu wengine zaidi ya wewe, watu
wapya.
Umoja hujengwa na kubomolewa, kwa pamoja tunaondoa yanayoweza kutusaidia
kutengana na kuharibu mahusiano.
Mahusiano hujengwa na hubomolewa, tunapokutana tunaondoa viambaza
vinavyotutenganisha.
Tumekubaliana kukutana ili kujenga.
MAHUSIANO NA VIONGOZI
Viongozi ni binadamu, ubinadamu sio liability ni asset.
Jifunze namna ya kuwasiliana na wengine, lugha unayotumia ukiumiza na wewe
utaumizwa tu.
Mkikosana tafuteni namna ya kumaliza kwa Amani na upendo.
Kiburi na majivuno yatakupeleka usikotaka lakini utaenda kwa kuwa kipofu wa macho ya
ndani yako.
Hakuna maoni: