3. KOSA LA SODOMA NA GOMORA.
06.04.2018
Yuda 1:7
"Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele."
Ni vema tukaelewa kuwa kuna kosa hili na namna ambavyo Mungu aliamua kuteketeza miji hii kwa moto na kumbukumbu yao kufutwa kabisa duniani mpaka leo. Sodoma na Gomora, kama ilivyo leo duniani, walifanya uasherati kwa kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili. Haya mambo ya mwili yasiyo ya asili ni yapi? Maana kama hujui asili ni wazi huwezi kujua feki. Kama ni uasherati wa kawaida isingeandikwa WALIFUATA MAMBO YA MWILI YASIYO YA ASILI.
Asili ni kama Mungu alivyoumba na kumfanya mwanaume na mwanamke kwa pamoja na kuwapa mipaka ya kuendenda kwao. Mwanaume kwa mwanamke na mwanamke kwa mwanaume na sio vinginevyo. Sodoma na Gomora, kama ilivyo leo hii, tunaona ushoga na usagaji ndio lugha ya dunia nzima mpaka imefika kiwango ambacho ukipingana na hao watu unaonekana wewe hufuati HAKI ZA BINADAMU. Huwezi kupewa misaada na nchi zilizoendelea kama wewe hukubaliani na ushoga au usagaji. HILI NDILO KOSA LA SODOMA NA GOMORA.
Kosa hili limeonekana sehemu nyingi sana kwenye biblia ikiwemo Mambo ya Walawi 18:22 na pia Warumi 1:18-32. Mambo ya Walawi inasema wazi kabisa kuwa usilale na mwanaume mfano wa kulala na mwanamke; NI CHUKIZO. Kwani biblia si hii moja tu? Mbona mataifa wanafanya ghasia kwa kutumia HAKI ZA BINADAMU? Ina maana leo HAKI ZA BINADAMU zimekuwa na nguvu juu ya NENO LA MUNGU ALIYE HAI? Nani kasema?
Waraka wa Paulo kwa Warumi unaonyesha kwanini mtu anaweza kufika kwenye kiwango cha kosa hili. Inaoneysha kuwa ni kwasababu kuna watu wanakuwa wameamua kupotosha kweli ya Mungu kwa uongo. Wanabadilisha uongo uonekane ukweli na ukweli uonekane uongo. Anaonyesha ni kwa kuwa watu hawa WAMEMKATAA MUNGU KATIKA FAHAMU ZAO ndio maana Mungu amewaacha waenende katika akili zao zisizofaa. Anaonyesha kuwa hata wanawake walibadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili, yaani usagaji na ushoga na kulawitiwa na mpaka sasa wapo wanaume ambao wanawalawiti wake zao na wanawake kwa ujinga wao na kuogopa kuachwa wanakubali kufanyiwa ISIVYO ASILI.
Fikiria mpaka wanaume wenyewe walipoacha asili ya kuwa na mwanamke na kufanya nae katika asili wakafanya makosa mawili makubwa. Kwanza wakaanza kuwalawiti wanawake, yaani kwenda nao kinyume na maumbile na asili ya kawaida, na pili wanaume wakawakiana tamaa wenyewe kwa wenyewe na kuanza kufanya ushoga ambao ni kunyume na maumbile ya mwanamke. BWANA AWAKEMEE KWA JINA LA YESU. Kosa la Sodoma na Gomora ndilo lilikuwa la mwisho kabla miji hii haijachomwa moto.
Angalia dunia yetu leo, angalia makanisani, serikalini dunia nzima, angalia ushoga na usagaji unavyopewa muda wa kutosha. Hawa watu wanakufuru mpaka wameamua kutumia UPINDE WA MVUA (RAINBOW) kuwa ndio rangi yao. Vijana mashuleni, vyuoni na hata makazini, wakurugenzi wa mashirika makubwa duniani na wapigania uhuru na haki za binadamu. Hawashtuki tu kuwa WANAPINGANA NA MUNGU? Kwa ajili ya haya, dunia itahukumiwa karibuni kama NENO LA MUNGU linavyoonyesha. Kama waliokosea kipindi kile hawakuachwa, sisi leo ni akina nani mpaka tujivune kuwa tuko juu ya Mungu? Angalia hili kosa.
Hili ni kosa la kwenda kinyume na maumbile na uumbaji na asili ya vile Mungu amefanya. Ni sawa na wale wanaojichubua na kumeza vidonge ili wawe wa kijivu badala ya kuwa wa njano. Ni wale wale. Ni sawa na wale wanaohangaika kubadili jinsia zao, wakaka wanataka wabadilishiwe viungo vyao viwe vya wadada ili na wao wabebe mimba kama wamama walivyo. HUU NI UPUMBAVU WA KIJINGA SANA. Na kwakweli BWANA AWAKEMEE WOTE. Huwezi kuelewa jambo hili mpaka likikupitia karibu au kwa mtoto wako au ndugu yako, ghafla uanze tu kumuona mkaka anaanza kuishi kidada, kujipodoa, kujipaka lipshine na lipstick. Hili ndo lilelile kosa la watu wanaonenepesha makalio na matiti yao.
Unadhani tuko salama kwa kiasi gani? Angalia jinsi ajenda hii ya uharibifu inavyoingizwa kwa watoto kupitia katuni mpaka na watoto wameanza kuona kumbe kuwa shoga na msagaji ni jambo la kawaida halafu wewe mzazi unawaachia tu watoto wako kuangalia katuni na vipindi vyote kwenye TV kwakuwa unawapenda sana? HUJUI UNALOFANYA WEWE MZAZI. BWANA AKUKEMEE KWA JINA LA YESU. Wazazi chunguzeni watoto wenu na hasa wakirudi toka shule za bweni au vyuoni, wengine huwa sio wao kabisa na huwezi kujua kama unajifanya unaenda kwa sayansi na teknolojia hii.
YKM: Satisfied In Jesus, Fulfilled In Christ.
God Incident Youth Camp 2018- GIYC2018
Theme: God Incident
Motto: God Awareness Matters
Key Verse: Psalms 100:3
Raphael JL
0787110003
Dodoma, Tanzania
Insta:@ raphaellyela
Youtube: Raphael JL
Web: www.ykm.or.tz
Hakuna maoni: