KANUNI ZA NGUVU
KANUNI ZA NGUVU
1. *Kumuelewa*; Jambo la msingi kwanza ni kumuelewa mtu. Kumuelewa kunaleta hali ya kumkubali. Mtu yoyote usiemuelewa ni vigumu sana kumkubali na hata kumuamini. *Kumuelewa maana yake kuwa na taarifa sahihi kuhusu yeye.*
2. *Kumkubali*, ni kama kusema ukishamuelewa ni lazima utaanza kumkubali na kadri unavyozidi kumuelewa ndivyo utakavyozidi kumkubali. Taarifa sahihi ambazo unazipata kuhusu mtu husika ndizo zinazokupa nguvu ya kuanza kuona kumbe ukweli ni nini na ndivyo kiwango chako cha kumkubali kinavoongezeka. Kumkubali ni kumchukulia kama ambavyo umemuelewa.
3. *Kumuamini*, ukishamuelewa na ukamkubali ni lazima sasa utaanza kumuamini. Ni vigumu sana uwe umemuelewa na umemkubali halafu usianze kumuamini na ndo maana katika kufahamiana, watu huanza kuambiana au kuulizana taarifa zao za kweli na sahihi ili mtu amuelewe mwingine na kisha waanze kukubaliana kwani lazima uaminifu utajengwa. Kumbe, *uaminifu unajengwa kwa kupata taarifa sahihi za mtu ambaye unakuwa umemkubali.*
4. *Kumpenda*, ni lazima utaanza kumpenda, ni lazima utampenda tu. Mtu ambae umeshamuelewa, ukamkubali na kumuamini ni lazima utampenda. Ni lazima utachagua kuweka hisia zako kwake kwa kiwango kikubwa sana. Maana sasa umeshamuamini. Uaminifu. Lakini sio kwamba umempenda tu hivi hivi bali umetoa muda wa kumsikiliza, kumfuatilia ili umuelewe, ukamuelewa na kumkubali na ukajikuta katika mchakato huo huo umeanza kumuamini. Lazima kinachofuata ni kumpenda. Ndivyo ilivyo. Haya mambo hayatokei tu, Mwl Makwaya husema KILA KITU KINATENGENEZWA.
5. *Kumtetea*, hawa ni mapacha, yaani kumtetea au kumpinga. Hayawezi kukaa pamoja. Huwezi kumtetea mtu ambaye hujamuelewa, na kwakuwa HUJAMUELEWA huwezi kumtetea mtu ambaye HUJAMKUBALI na kwakuwa hujamkubali huwezi kumtetea mtu ambaye HUJAMUAMINI na hiyo inamaanisha huwezi kumtetea mtu ambaye HUJAMPENDA. Wewe pima tu wale watu unaowatetea, ni lazima kuna namna umevuka kwenye hizi kanuni zote nne. Ni hatari kumtetea mtu ambaye kanuni hizi haziko halisi kwako. Hii ndio sababu watu huwatetea watu wao. Unajiuliza kwanini unampiga mwingine?
6. *Kumpinga*, ni pacha wa kanuni namba tano. Kumpinga ni maamuzi, haiwezi kutokea tu. Ili umpinge mtu vizuri ni lazima kanuni ya kwanza mpaka ya nne ziwe hazipo au ziwe kinyumenyume. Utampinga tu kama humuelewi. Kama humkubali. Kama humpendi. Kama humuamini. Unaweza hata ukapima wewe mwenyewe, ukajiuliza, kwanini unampinga unayempinga? Inawezekana hujaelewa anachofundisha au anavyofundisha. Kwa namna yoyote ile ni lazima kanuni ya kwanza ianze. Na hii ni kazi ya taarifa.
Kila kanuni moja kati ya hizi ina nguvu yake lakini zote zimeshikana sana. Dunia nzima watu wanatafuta kujua taarifa sahihi za watu. Wapelelezi duniani, iwe ni kwa mtu binafsi au nchi huwa wanatafuta kujua taarifa sahihi za watu na wakizijua huzitumia sawa na nia yao ya ndani. Hii ndio maana lazima uwe makini sana kusema mambo yako kwa mtu maana hata wale manabii wa uongo wanatafuta hicho tu. MWENYE KUJUA TAARIFA SAHIHI ANA NGUVU SANA. Wakati mwingine tutajifunza KANUNI YA KUPIMA UBORA WA TAARIFA.
Hizi ni kanuni za nguvu kwani zina uwezo wa kusababisha mambo mazuri au mabaya kutokea kwenye maisha ya mtu husika. Hii inamaanisha kuwa mtu ambaye anakuwa ametimiza kanuni zote nne, matokeo yake ni kanuni mbili za mwisho. Aidha utapingwa au utatetewa. Kila mtu anao uchaguzi huu wa kufanya hivi, yaani uchaguzi wa kuamua nani wa kumtetea au kumpinga. Na ni kama kila mtu ana mtu anayempinga au kumtetea hata kama atajifanya yeye hana adui, hapo mimi sijaongelea uadui. Unaweza kumpinga mtu na asiwe adui yako.
God Incident Youth Camp 2018-GIYC2018
Theme: GOD INCIDENT.
Motto: God Awareness Matters!
Key verse: Psalms 100:3.
YKM: Satisfied in Jesus, Fulfilled in Christ!
Raphael Joachim Lyela
0767033300 (Whatsapp tu)
Dodoma,Tanzania.
Instagram: @raphaellyela
YouTube: Raphael JL
Web: www.ykm.or.tz
Hakuna maoni: