KOTI LA UPUPU, KINACHOWASHA SIO KOTI NI UPUPU.
Isaya 54:15
*Tazama, yamkini watakusanyana; lakini si kwa shauri langu. Watu wowote watakaokusanyana juu yako wataanguka kwa ajili yako.*
Kuna msemo unasema "ADUI WA ADUI YANGU NI RAFIKI YANGU", hii ni mpaka mkubaliane ili kila mmoja achague upande upi anaenda ili kusaidia kumshinda adui yake. Ukiwa unakimbizwa na simba, njiani ukakutana na mtu anakimbizwa na ANAKONDA, lazima mtashirikiana kukimbia upande mmoja na hata ikibidi kujipanga kwa pamoja kuwashinda maadui wenu, ingawa kila mmoja ana adui yake. Hii ni tofauti kidogo. Fikiria wewe una adui, wa hiari au wa kutengeneza au kutengenezwa, halafu siku moja ukakutana na mtu akimsema vibaya yule adui yako. Kuna namna utaanza kujisikia vizuri na kuona kuwa huyu adui wa adui yako anaweza na anafaa kabisa kuwa rafiki yako ukiamua.
Kuna watu hujiamulia tu na kujitolea kuwa adui wa mtu. Kuna wengine ni maadui waliotengenezwa na watu wengine, na wengine ni maadui waliojitengeneza na pia wapo maadui waliotengenezwa na adui mwenyewe, iwe kwa kujua au kutokujua. Vyovyote vile ilivyo adui mzuri ni yule aliyejiamualia; aliyetenegenezwa na watu wengine maana huyu ni adui wa ajabu sana. Bila kujali haya yote, kila adui ana fursa ya kupendwa, WAPENDENI ADUI ZENU. Ugumu wa kumpenda adui yako unafanana sana na urahisi wa kumpata adui. Wewe kaa ufikirie vizuri, labda uko ofisini na unafanya kazi na watu kadhaa, kadri unavyosimamia haki na sheria ndivyo watu watakavyoendelea kukuona wewe ni adui. Uadui unatengenezwa, kama mengi yanayotengenezwa.
Ulishawahi kumkubatia mtu aliyevaa koti la upupu ila wewe hujui?
God Incident Youth Camp 2018-GIYC2018
Theme: GOD INCIDENT.
Motto God Awareness Matters.
Key verse: Psalms 100:3.
YKM: Satisfied in Jesus, Fulfilled in Christ!
By Raphael Joachim Lyela
0787110003
Dodoma,Tanzania.
Instagram: @raphaellyela
YouTube: Raphael JL:
Web: www.ykm.or.tz
Hakuna maoni: