Ads Top

LUCIFER BIN SHETANI: UKWELI MGUMU MTAMU KAMA UTAULA KWANZA.



Neno Lucifer au Lusifa ni jina. Shetani pia ni jina. Uhusiano uliopo hapa ni wa lugha na mantiki lakini ni kitu kile kile. Lucifer ni neno la KILATINI linalomaanisha LIGHT BEARER au MBEBA NURU au MWANGA au NYOTA YA ASUBUHI na kwa tafsiri hii maana yake MBEBA MAARIFA, au KNOWLEDGE BEARER. Neno hili lipo Isaya 14:12 kwa biblia kadhaa za lugha ya kingereza, kwa Kiswahili inaweza kuwa ngumu kulipata neno hili. Kwahiyo neno Lucifer sio la Kiebrania, kumbuka agano la kale liliandikwa kwa asilimia kubwa kiebrania. Lakini pia agano jipya limeandikwa kwa lugha ya kiebrania na kigiriki kwa asilimia kubwa, kwahiyo huwezi kukutana neno Lusifa kwenye agano jipya.

Neno Shetani au SATAN ni neno la kiebrania lenye maana ya ADVESARY au mpinzani au adui anaepinga ambalo ni neno HELEL ambalo ndio Lucifer kwa kilatini. Ni kitu  kile kile ila kwa macho tofauti. Na ndio maana kumekuwa na changamoto ya kuelewa sana kuhusu LUCIFER. Ukisoma biblia utagundua kuwa biblia imetoa sifa kadhaa kwa shetani, pengine inamuita LILE JOKAA LA ZAMANI au LEIWATHANI au MUOVU. Kikubwa hapa ni kujua kuwa ni kitu kile kile.
Nadhani swali kubwa lililopo hapa ni lile linalosema, *LUCIFER ALIKUWA KIONGOZI WA SIFA MBINGUNI? Halafu akaja akatupwa duniani?*

Mfululizo huu utakujia na majibu.
Fuatilia Instagram account yangu kujifunza hili.

YKM: Satisfied In Jesus Fulfilled In Christ

Raphael JL
+255 787110003
Dodoma, Tanzania

Insta: @raphaellyela
Youtube: Raphael JL
Web: www.ykm.or.tz
Www.fichuka.blogspot.com

Maoni 1 :

  1. naitaji kusoma bibilia ya lusifaa

    JibuFuta

Inaendeshwa na Blogger.