Ads Top

MAAMUZI YA KUTAFAKARI SHUHUDA ZA BWANA.



05.04.2018
Mkate wa siku
Zaburi 119:95
“Wasio haki wameniotea ili kunipoteza, nitazitafakari shuhuda zako”

Ukweli ni huu, kwamba maadui zetu na watu wasiotupenda wala kutuwazia mema, watu wanaotamani na kutaka kutuona tumeanguka hata leo hawataacha kutuotea. Hawataacha kututegea mitego. Hawataacha kutuchunguza na kuona kuenenda kwetu. Hawataacha kutuwekea viunzi mbele yetu. Hili halitakiwi kuwa geni kwetu, wala halitakiwi kututisha kwa namna yoyote. *Nguvu yetu haitokani na vitisho vyao*. Lazima na sisi kwa upande wetu tuamue.

Kama mzaburi anavyoweka wazi, wasio haki wanamuotea ili kumpoteza lakini yeye amefanya kuamua kuzitafakari shuhuda za BWANA. Ameamua kuachana na vitisho vya maadui na kutafakari matendo makuu ya Mungu. Sio kwamba maadui wameondoka au wameacha kutishia, hapana. Bali mwenye haki ameamua KUWAPUUZIA NA KUMZINGATIA MUNGU NA SHUHUDA ZAKE. Hii inampa nguvu sana mtu wa Mungu maana sasa ndani yake kunajengeka msaada upatikanao wakati wa mateso na matisho kama hayo. Hata wewe leo unaweza kuchagua jambo hilo, ukaamua kuwapuuzia maadui zako na kuzitafakari shuhuda za BWANA.


YKM: Satisfied in Jesus, Fulfilled in Christ!

God Incident Youth Camp 2018-GIYC2018
Theme:      GOD INCIDENT.
Motto:      God Awareness Matters.
Key verse: Zaburi 100:3.

Raphael Joachim Lyela
0787110003
Dodoma,Tanzania.

Insta: @raphaellyela
YouTube: Raphael JL
Web: www.ykm.or.tz

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.