MAISHA YA KUSUBIRI NYOTA IKUTABIRIE. (ASANTE UJINGA)
Hata leo kuna watu wanasubiria wanunue magazeti ili waangalie nyota zao zinasemaje, wanasubiria ziwaambie nguo za kuvaa, njia za kupita, watu wa kusalimiana nao, chakula cha kula leo na hata watu wa kuamua kuwaelewa. Wapo wanapokea barua pepe kwenye mitandao wakipewa unabii na kutabiriwa kuhusu kazi zao, mahusiano yao, tabia zao na hata vyakula vyao. Maisha ya kuongozwa na nyota ni maisha ya kuongozwa na nguvu za giza. Ni sawa na maisha ya kufanya YOGA tu. Asili ya kitu ndio roho yake na kwa hiyo huwezi kubadilisha asili njiani ni lazima ukabadili asili kwenye asili yake. Ila kwakuwa watu wanapenda ubishi na wanapenda kuiga kila kitu IPO SIKU TUTAIGA MPAKA KUPUMUA.
Leo lipo neno la Mungu kwa ajili yako, ila hutaki sauti ya Mungu na badala yake unataka UNABII WA NYOTA, sijui aries, scorpio, nk. *Zodiac na mambo yote ya unajimu ni uchawi wa kiwango cha juu maana huwa wanapatia kwenye baadhi ya vitu.* KUPATIA SIO USAHIHI. Mbona waganga wa kienyeji wanapatia na watu wanaenda huko kwa shughuli zao za kisiasa na biashara, je hiyo inawafanya waganga wa kienyeji kuwa wa Mungu? Yaani kweli, unaamua kumuacha Mungu aliyekuumba, na kumpa heshima inayostahili unaenda KUVIABUDU VIUMBE. Unaikubalia nyota inavyosema kuliko aliyeiumba nyota yenyewe?
JINGAS MINISTRY.
Note:
Hata kama anayefanya hivyo ni baba au mama yako wa kimwili sijui wa kiroho, au ni rafiki yako sana au ni mtu maarufu sana ambaye amechora kabisa TATOO ya nyota yake kwenye mapaja yake BADO SIO SAWA.
Kumbuka wewe ni wewe, uko peke yako na wewe ni wa pekee, wewe sio kila mtu.
LINDA UTAMBULISHO WAKO KATIKA KRISTO.
YKM: Satisfied In Jesus Fulfilled In Christ
Raphael JL
+255 787110003
Dodoma, Tanzania
Insta: @raphaellyela
Youtube: Raphael JL
Web: www.ykm.or.tz
Www.fichuka.blogspot.com
Hakuna maoni: