Ads Top

TOFAUTI KATI YA MSANII WA NYIMBO ZA INJILI(GOSPEL ARTIST) NA MWABUDU (WORSHIPER)


Qn: *Kuna Tofauti gani kati ya Msanii wa Nyimbo za Injili 'Gospel Artist' na Mwabudu 'Worshipper'??*

Na Pst. Raphael JL
[PART 1]

📍 Wasanii wa Nyimbo za Injili 'Gospel Artists' wana akili za sokoni, yaani, akili za kuangalia soko linasemaje ndipo atoe wimbo wake au afanye 'shooting' inayotafsiri huo usanii wenyewe.
Waabudu 'Worshippers' wana akili za MUNGU.

📍 Ni msanii, kwa hiyo USANII una nguvu kwenye anayoyafanya yeye; *Mwenendo* wake ni wa kisanii, *Mavazi* yake ni ya kisanii.

📍 USANII una uhusiano na MASHINDANO, Hivyo kuna namna anafanya vitu kwa mashindano ili awafunike wengine.

📍 Usanii una tabia ya kutafuta KUJULIKANA NA UMAARUFU.

📍 Msanii 'Gospel Artist' hajali mambo ya msingi; *MAHUSIANO YAKE NA MUNGU SIO MUHIMU SANA KULIKO KIPAJI* Wasanii wengi wa hivi wanaishi kwa KIPAJI na ndiyo maana wanaweza kujichanganya na MADISKO na bado wakasimama Jumapili kanisani.

📍 Msanii wa Gospel hana haja ya *KULIJAZA NENO LA MUNGU NDANI YAKE* kwani anategemea sana kipaji chake. Hata nyimbo, ukizisikia zimekaa kisokosoko tu, upande bongo flava na upande ule Yesu Yesu kwa mbali. Ila nyimbo zao, wao wenyewe husemwa ~*ZINAPENDWA NA KILA MTU kwani wameitwa kuhubiri Injili kwa njia ya uimbaji*'~
Kwao watu ni wa muhimu sana kujali wanachotaka kuliko Mungu.

📍 Msanii huyu akiwa kiongozi wa THE SO CALLED PRAISE AND WORSHIP...atawafanyisha mazoezi kanisani mpaka mmkubali; Atawanyanyulisha mikono kama atakavyo; Atawaamuru kufanya ANACHOTAKA YEYE mpaka mtaelewa tu kwa ujumla....MOST OF THEM USE EMOTIONS IN PLACE OF THE PRESENCE OF GOD.

📍 Wasanii huwa wanakwazika sana wasiposifiwa au kuonyeshwa kama wanajulikana mahali wanakokwenda maana wao UMAARUFU NI MUHIMU SANA HATA KAMA HAWANA HELA.

📍 Wasanii wengi hutunga nyimbo zao kwa kuangalia mahitaji ya soko au upepo wa soko la mziki wenyewe wa injili na kwasababu hiyo wanakuwa *watumwa wa soko na sio Mungu mwenyewe.* Na ndio maana DUNIA imewaandalia MASHINDANO NA TUZO AU AWARDS.
📍 Maisha ya MATUKIO, EVENTS ndo huwasukuma sana maana wanapenda kuonekana, *they want to be everywhere angalau all the time if possible*...
Kama ni wakaka wana nguo zao huwa wanavaa na ukimuona tu unajua umekutana na msanii...vitu vingi ni feki....wadada ndo huwa wahanga zaidi

📍 *Maisha ya ibada kwa msanii sio muhimu sana, so anaweza kuwa anapiga punyetto na bado akawa na ujasiri wa wa kushika keys Jumapili.*

📍Akili zao ni MATUKIO so UWEPO WA MUNGU kwao HUWA MWINGI KANISANI na uwepo wenyewe ni wa KUUNGANISHA kwani lazima AVUTE KWANZA uwepo kwa kuimba.

GOD IS LOOKING FOR TRUE WORSHIPERS

YKM: Satisfied In Christ

Raphael JL
0787110003
Dodoma, Tanzania

Maoni 1 :

  1. Asante sana kwa Mafundisho mazuri Pastor,
    Hivi karibuni imefika nchini (TUZO ZA GOSPEL) kwa nchi zilizoendelea imekuwepo toka miaka ya 1938 kama Stela awards, SABC Awards Grammy's awards na wakristo wahudumu hupewa tuzo na huzipokea ..Je wao tuwaite wasaniii was Gospel ama wahudumu.

    JibuFuta

Inaendeshwa na Blogger.