Ads Top

UKAMILIFU NI MUNGU MENGINE YOTE YANA MWISHO WAKE.


06.04.2018
Mkate wa siku
Zaburi 119:96
Nimeona ukamilifu wote kuwa na mwisho, Bali agizo lako ni pana mno.

Mzaburi anatukumbusha tena kwenye mkate huu wa uzima wa siku ya leo kuwa ameona ukamilifu wote kuwa na mwisho, bali agizo la Bwana ni pana mno. Hii ndio kweli. Ukamilifu mwingine wowote ule una mipaka na mwisho wake. Hauwezi ukaenda zaidi ya ulivyotakiwa kwenda au kufanya. Uzuri una mwisho na mpaka wake. Nje ya Mungu, hakuna utimilifu wenye manufaa na faida kwa mwanadamu. Utoshelevu uko ndani ya NENO LA MUNGU.

Ni kweli pia kwamba agizo la BWANA au neno lake ni pana mno, mno kwa maana ya kutouwa na mwisho na mipaka. Kama ambayo imeandikwa, mambo mengine yote yatapita lakini NENO LA MUNGU litasimama na kudumu milele. Kwanini kutaabishwa na mambo ambayo yana mwisho wake?  Kwanini kusumbuliwa na vitu ambavyo unajua kabisa vinapita na kupotea wakati kuna neno la Mungu na maagizo yake yanayodumu milele yote?

Ila ni lazima kila mmoja wetu atafsiri nini maana au nini ndio ukamilifu wake. Yaani ukipata nini au ukienda wapi au ukiona nini au ukiwa na nani unajiona UMEKAMILIKA? Ukiwa kwenye hali gani, ukielewa nini, ukimiliki nini, ukifanya jambo gani unajiona umepata UKAMILIFU? Hayo yote yanapita. Yana mwisho, yana mipaka. Hayadumu. Maana yake sio ya kuyategemea. UKAMILIFU NI NENO LA MUNGU. UKAMILIFU NI MUNGU MWENYEWE. UKAMILIFU NI KUWA NA MUNGU. Huu ndio ukweli hata kama hauvutii sana. Dunia ya leo imejaa kila aina ya mambo yenye lengo la kumuondoa Mungu kwenye akili za watu, kila kitu cha kiMungu au chenye Mungu, iwe ni mtu au kitu ni lazima kitapigwa vita kali sana. Lengo ni lile lile, kumtoa Mungu asionekane kuwa ndiye aliyetenda yote tunayoona n ahata tusiyoona. Ili kuruhusu elimu za kibindamu kama za akina Karl Max na Cherles Darwin kuonekana kuwa ndio sahihi kwamba mwanadamu alikuwa Sokwe. Unahitaji kuwa na akili zilizolemaa kuamini kitu kama hicho maana historia itakuwa haiwatendei haki wale sokwe wa Gombe.

Yote katika yote,YESU NI BWANA NA UKAMILIFU WOTE UKO NDANI YAKE.


God Incident Youth Camp 2018-GIYC2018
Theme:GOD INCIDENT...
Motto God Awareness Matters....
Key verse Zaburi 100:3.

YKM: Satisfied in Jesus, Fulfilled in Christ!

By Raphael Joachim Lyela
Web: www.ykm.or.tz
0787110003
Dodoma,Tanzania.....
Instagram: @raphaellyela
YouTube: Raphael JL:

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.