KOSA LA KORA
AINA ZA MAKOSA YAKUWA NAYO MAKINI
7. KOSA LA KORA
Tunaendelea na mafundisho yetu ya aina za makosa ya kuwa nayo makini kama tunavyojifunza kwenye kitabu cha Yuda. Na tayari tumeshajifunza makosa kadha ikiwemo kosa la wana wa Israel baada ya kutoka Mistri, Kosa la Sodoma na Gomora, kosa la Baalam na leo tuangalie kosa namba 7 ambalo ni la mwisho. Unawea ukasoma makosa yote kwenye *www.fichuka.blogspot.com* pamoja na masomo mengine pia.
Kosa la kora limeandikwa kwa uzuri sana kwenye kitabu cha Hesabu 16. Kora alimuonea wivu Musa na akamtakia maneno magumu sana. Alimuona Musa kama mtu anaejiinua na kujitukuza na kujifanya yeye tu ndiye nabii au ndiye mtu anayesema na Mungu peke yake. Musa alipopata hayo maneno aliumia sana. Kibaya zaidi ni kwamba Kora alikuwa kama mtu mwenye ushawishi anayeweza kuwavuta na wengine pia waasi mamlaka iliyopo. Kwahiyo hakuwa peke yake ingawaje yeye ndo alikuwa kiongozi wao. Kora alikuwa mlalamishi sana, alimlaumu sana Musa kuwatoa Misri na kuwaleta kwenye nchi iliyojaa asali na maziwa kwa lengo la kuwaua. Alimlalamikia sana Musa. Kumbuka kosa la kwanza la mfululizo wa Makala hii.
Malalamiko na malaumu ya Kora na watu wake yalimfanya Musa aongee na Mungu na kumuomba ajidhihirishe kwa wana wa Israel ili nabii wa kweli wa Mungu aonekane. Na ndipo tunasoma habari ambayo haijawahi kutokea tangu dunia iumbwe. Ardhi kupasuka na kuwameza akina Kora na jamaa zake wote wakiwa hai na kisha ardhi kujifunika kwa mkono wa Bwana mwenyewe. Ni rahisi kudhani ilikuwa kawaida, wewe fikiria tu ungefanyaje kama ungekuwa unayaona hayo? Kumbe kosa la Kora ni kosa la UASI na kuwashawishi wengine waasi kinyume na MAMLAKA YA MUNGU mahali fulani. Inawezekana kuna Kora kwenye familia, kazini, kwenye makundi ya WHATSAPP nk. Inawezekana mwingine ndo Kora wako au wewe ni Kora wa mwingine. Kikubwa ni kujua nafasi yako na kukaa hapo.
Ridhika na nafasi yako, kumbuka lile kosa la pili la malaika wasiokaa katika enzi yao wenyewe. Tulia hapo kwenye nafasi yako. Acha wivu. *Fahamu kuwa kila mtu amepewa kwa sehemu, tunajua kwa sehemu, tunafundisha kwa sehemu, tunahubiri kwa sehemu, tunatabiri kwa sehemu, tunatoa unabii kwa sehemu.* Kila mtu amepewa talanta sawa na uwezo alionao wa kuifanya ile talanta IMZALIE MUNGU MATUNDA. Wivu wa namna hii ni hatari sana. Ni kweli sasa hivi hatuoni ardhi ikipasuka na kuwameza watu lakini Mungu atusaidie na kuturehemu sana yasitukute haya. Hii ndio siri ya MASHINDANO, kutokuridhika. Usiporidhika na ulivyonavyo utashindana mpaka na Mungu mwenyewe. BE VERY CAREFUL.
Ukimuona Kora wako, wewe kisikusumbue, simama na Mungu. Mungu atamfundisha somo kama anafundishika. Usilipize kisasi. Usitake mashindano. Wewe kaa na Mungu vizuri. HESHIMA YA MTUMISHI WA MUNGU WA KWELI INATOKA KWA MUNGU MWENYEWE.
YKM: Satisfied In Jesus, Fulfilled In Christ.
Raphael JL
+255 78710003
Dodoma, Tanzania
Insta: @raphaellyela
Youtube: Raphael JL
Web: www.ykm.or.tz
Www.fichuka.blogspot.com
Hakuna maoni: