KOSA LA KUUTIA MWILI UNAJISI KWA NDOTO
AINA ZA MAKOSA YAKUWA NAYO MAKINI
Tunaendelea na mafundisho yetu ya aina za makosa ya kuwa nayo makini kama tunavyojifunza kwenye kitabu cha Yuda. Na tayari tumeshajifunza makosa kadhaa ikiwemo *kosa la wana wa Israel baada ya kutoka Misri*, *Kosa la Sodoma na Gomora,* *kosa la Baalam* na leo tuangalie kosa namba 4. Unawea ukasoma makosa yote kwenye *www.fichuka.blogspot.com* pamoja na masomo mengine pia.
Huenda ukaona ni kitu cha kawaida sana lakini sio cha kawaida kulala na usiku unaota unafanya tendo la ndoa iwe na mtu unayemfahamu au na mtu usiyemfahamu. Wakati mwingine unaweza ukaota kabisa ni viumbe vya ajabu. Unaamka unajikuta umejichafua na manii kana kwamba ulikuwa unafanya ngono kabisa. Ukiliangalia kosa hili sio kosa la kawaida kwani lina maana kubwa sana katika maisha ya kila siku. Swali la kujuliza ni *kwanini hali hiyo itokee na huku umelala?* Ni muhimu kujua kuwa ukiwa umelala, mwili unakuwa katika hali ya kufa ila roho inakuwa inaona na kuelewa yanayoendelea na ndio maana ya ndoto pia. Ndoto ni njia pia ya kuyaona mambo ya rohoni.
Kwa hiyo kama kujichafua huko kumetokea wakati wa ndoto ni sawa kabisa kuona na kusema kuwa lazima kuna mambo yanayoendelea kwenye ulimwengu wa roho ambayo yanaathiriwa na mambo ya mwili. Nikupe mfano, kama wewe ni PORN ADICT au umeathiriwa na kuangalia picha za ngono, au unapenda kuangalia movie zenye mambo hayo ni rahisi sana kujikuta unaishi maisha ya namna hii. Hii ina maanisha kuwa mambo unayoruhusu kuingia ndani ya moyo wako yanaweza kujirudia hata ukiwa umelala. Hii ni moja.
Pili, kuota ndoto za namna hii inaweza kabisa ikawa ishara kwamba wewe una mahusiano ya kiroho na nguvu hizi za giza kwani kwa utaratibu wa asili wa uumbaji wa Mungu haitakiwi kuwa hivyo. Kwahiyo inawezekana kabisa kuwa hilo jambo linatokea kama dalili kwamba inawezekana upo katika mwenendo unaosababisha mambo hayo yanayokujia. Unaamka unajikuta umechafuka, umechafua mwili, umelichafua hekalu.
Njia ya kutoka na kushinda katika hali hii
💡Ni kuomba msaada wa Mungu.
💡Ni kutambua kuwa wewe kwa jitihada zako huwezi.
💡Ni kujikabidhi kwa Bwana Yesu na kuomba neema ya kuishi maisha matakatifu.
💡Ni kuwa na ushirika na neno la Mungu kila siku.
💡Ni kuwa na ushirika na Roho Mtakatifu kila siku.
💡Ni kuwa makini na kuweka mipaka ya mambo ambayo milango yako mitano ya fahamu inayachakata kila siku.
Anayeweza kukusaidia ni Yesu pekee. Hivyo kama hujaokoka ni vyema ukafanya hivyo na kama umeokoka ina maanisha kuna vitu havijakaa sawa, hebu jichunguze. Msaada unapatikana MSALABANI masaa 24 kwa siku zote 7.
YKM: Satisfied inJesus, Fulfilled in christ
Raphael JL
+255 787110003
Dodoma, Tanzania
Insta: @raphaellyela
Youtube: Raphael JL
Web: www.ykm.or.tz
Www.fichuka.blogspot.com
Hakuna maoni: