Ads Top

KUKEMEA


KUKEMEA

03.05.2018

Hosea 4:6
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.
My people are destroyed for lack of knowledge: because thou hast rejected knowledge, I will also reject thee, that thou shalt be no priest to me: seeing thou hast forgotten the law of thy God, I will also forget thy children.

Mithali 1:7

Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.
The fear of the LORD is the beginning of knowledge: but fools despise wisdom and instruction.

MAARIFA NI UJUZI WA JUMLA UNAOTOKA KWENYE NENO LA MUNGU

Waefeso 6 : 11 - Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.

NDO MAANA UNAKEMEA WEEEE NA BADO HALI IKO PALE PALE...

KUNA SIRI KUBWA SANA HAPO

RESIST THE DEVIL AND HE SHALL FLEE.YAANI HAKUNA NAMNA UKIMPINGA ATAKAA

YESU ALIMPINGAJE SHETANI? -ALITUMIA NENO

👉🏽 HUWEZI KUMPINGA SHETANI KWA MAOMBI NA MBWEMBWE ZA KUKEMEA
👉🏽 KAMA HAKUNA NENO HUMUWEZI SHETANI
 👉🏽SHETANI ANAPINGWA KWA NENO LA MUNGU, MPINGENI KWA NENO NAE ATAWAKIMBIA
 👉🏽VAENI SILAHA ZOTE ZA MUNGU ILI MUWEZE KUZIPINGA....NENO NI LAZIMA

VITA INAANZA KUPIGANWA KWENYE MIND-UFAHAMU-NENO KABLA HATA HUJAENDA KWENYE UWANJA WA VITA. BILA NENO UNAPIGANA VITA GANI?

Hebu angalia Efeso 6:11 upya....

1.VAA SILAHA ZOTE ZA MUNGU....HUWEZI KUZIVAA KAMA HUZIJUI..UKIZIJUE UJUE MAANA YA KUZIVAA NI NINI.

2.KUZIPINGA HILA ZA SHETANI....LAZIMA UJUE VITA HII INAPIGANWA WAPI ILI HATA UNAPOAMBIWA UNAINGIA KWENYE MAOMBI YAO YA VITA UJUE NI NINI UNAFANYA

HUWEZI KUMPINGA SHETANI KWA MANENO YAKO YA UBUNIFU

13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
14 Basi simameni, *hali mmejifunga kweli viunoni,* na kuvaa *dirii ya haki kifuani,*
15 na kufungiwa miguu *utayari tupatao kwa Injili ya amani;*
16 zaidi ya yote mkiitwaa *ngao ya imani*, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.
17 Tena ipokeeni *chapeo ya wokovu, na  *upanga wa Roho* ambao ni *neno la Mungu;*
18 kwa *sala zote na maombi* mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;

 'Waefeso 6:13-14-15-16-17-18'


SWALI SASA: UNAENDAJE VITANI NA HIZO SILAHA ZOTE?

Raphael Joachim Lyela
Web: www.ykm.or.tz
0787-110003
Dodoma,Tanzania
Instagram: @raphaellyela
YouTube: Raphael JL

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.