Ads Top

MUHTASARI WA KITABU CHA WARUMI.



MUHTASARI WA KITABU CHA WARUMI.
☀☀☀☀☀☀☀☀☀☀☀☀☀☀☀☀

UTANGULIZI

Kina Sura 16
Kina Mistari 433

*Dhima/somo kuu: HAKI YA MUNGU IMEDHIHIRISHWA* Mwaka Wa kuandikwa: 56 - 58B.K
Mahali: Korintho
Mwandishi: Paulo
Barua ya 6 ya Paulo.

*WARAKA/BARUA YENYEWE!*
Barua hii ya kitheologia zaidi yenye kuvutia na ndefu kuliko zote inaonyesha shauku yake ya kutaka kuufikia ulimwengu wote, kwa kufika hapa Rumi mji mkuu Wa dola la Rumi iliyokuwa inatawala ulaya yote, kaskazini mwa Afrika na pande za Asia. 􀊕Alipotimiza azma yake, bado Paulo alitamani kufika hadi Uhispania!
􀌛Wakati Wa kuandika kuelekea mwisho Wa safari yake ya 3 ya kimisionari, Paulo alikuwa Korintho kama mgeni katika Nyumba ya Gayo, alipotaka kuwa akiandika Waraka huu kwa njia ya msaidizi wake Tertio. Paulo anaandika waraka wake kwa muundo Wa maswali na majibu au mtindo Wa
majadiliano akijadili "haki" ya Mungu, asili ya dhambi, akitoa nukuu kadha Wa kadha Agano la kale akilinganisha na maana sahihi ya Agano Jipya.
􀀑Kwenye kitabu hiki anaongelea dhambi na haki kupitia maana zenye kina na mapana ya ufafanuzi za agano la kale kuanzia:
􀅞Abrahamu, Daudi, Adamu, Sara, Rebeka, Yakobo na Esau, Farao na pia ahadi alizopewa Israeli na namna gani Wakristo wanaweza kuenenda katika imani.
􀅣 Paulo aliandika kwa mji mkuu bila kutambua kuwa alikuwa akiuandikia ulimwengu mzima na vizazi vyote vya wanadamu!

Mwisho!
Historia inaonyesha kuwa kupitia waraka kwa warumi "mwenye haki ataishi imani", Martin Luther, Kavini, Wesley waliwasha moto wa mageuzi na
uamsho (Reinnances & Reformation) huko ulaya baada ya kipindi kirefu cha Giza, Kuikumba ulaya

YKM: Fulfilled In Jesus, Satisfied In Christ

Raphael JL
+255 78710003
Dodoma, Tanzania

Insta: @raphaellyela
Youtube: Raphael JL
Web: www.ykm.or.tz
Www.fichuka.blogspot.com

Maoni 2 :

Inaendeshwa na Blogger.