Ads Top

UGONJWA WA KUMPENDA MUNGU,MZIZI WA BIDII YA MWENYE MAARIFA.


UGONJWA WA KUMPENDA MUNGU, MZIZI WA BIDII YA MWENYE MAARIFA

Lazima shida ni kumpenda Mungu. Huu ndio mzizi wa bidi ya wenye maarifa. Kumpenda Mungu. Mungu mwenye naamini anajua hii shida mpaka anasema tumpende kwa mioyo yetu na nguvu zetu zote na akili na kila kitu. Huu ni kama sio ule upendo wa mdomoni maana mahali pengine anasema mnanipenda kwa maneno lakini mioyo yenu iko mbali name. lazima shida ni kumpenda Mungu. Mambo yote tunayoyapenda yanakuwa ni kipaumbele na pia bidi yetu itaelekezwa huko. Bidii inahitaji maarifa ili izae matunda mazuri lakini inahitaji upendo ili ifike mbali na iwe na nguvu. Ndo maana shauku inapungua maana shauku kwa kitu au mtu usiempenda ni maumivu ya kuvumilia adui afe lakini unaona miaka inaenda na kurudi tu.

Upendo haujifichi. Kuna namna ya kujivunia kumpenda au kupendwa nae. Upendo huu unasukuma shauku na bidii yetu katika kutenda na kufanya yote yanayoonyesha kuwa tunapenda. Angalia Yohana 3:16, KWA MAANA JINSI HII MUNGU ALIUPENDA ULIMWENGU, ni wazi kuwa alionyesha na kuthibitisha kule kupenda kwake, akatoa. Na sisi tunaonyesha na kuthibitisha kumpenda kwetu na kuitikia upendo wake kwetu kwa KUMTII na kutoa mengi tu ndani ya maisha yetu. Kumpe, kwa maana ya kawaida tu, kupenda kunalazimisha kutoa na kunahitaji utii. Hujiulizi kutoa kwani upendo unataka hicho, unataka kutoa. Mungu Baba yetu alimtoa mwanae, nini anatunyima? Warumi 8:32 inasema wazi kabisa ukisoma kuwa Mungu HAKUMZUILIA MWANAE, AKAMWACHILIA NA KUMTOA KWA AJILI YETU, ATAKOSAJE KUTUKIRIMIA NA MAMBO YOTE PAMOJA NAE?

Mahali pengine biblia inasema yeye alitupenda kwanza, nasi tunajifunza kumpenda kwakuwa tumefundishwa nay eye. Hatujui kupenda. Hatujawahi kupenda mpaka Mungu alipotupenda. Na alipotupenda akamtoa mwanae atufie ili tuokolewe kwa neema yake. Ni upendo wa namna gani huu, mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake? Yohana 15:13, hakika hakuna upendo mkuu na mkubwa namna hii, MTU KUUTOA UHAI WAKE KWA AJILI YA RAFIKI ZAKE. Tumependwa jamani. Tuna ushahidi wa upendo wa Mungu mpaka hatuwezi hata kueleza. Nini anataka kwetu? Kwamba tumpende na kumtii. Tumpende kwa hali zetu na vile tulivyo maana sisi hatuwezi kufa kwa ajili yake ili tumuokoe. Hapa sasa.

Kama ukimpenda mtu kuna vitu unafanya na kuonyesha, vipi ukimpenda Mungu ambaye thamani yake hailingani wala kufanana na mtu mwinginewe? Tutaoa pia, muda wetu, nguvu zetu na akili zetu. Hapa siongelei kupima kama unampenda Mungu kwa kuhudhuria matamasha ya uimbaji na muziki na huduma za kucheza. Songelei mambo yanayoonekana kwa nje na watu wengi, hapana. Naongelea upendo wa mtu binafsi ndani ya moyo wake. Namna anavyomtafuta na kumlingana BWANA kwa bidi na mapenzi ya moyo wake kila siku. Bila kusukumwa, bila kupangiwa ratiba ya maombi, bila kuonekana na mtu mwingine, bila kushindanishwa, bila kuhimizwa kwa namna yoyote.

Naongelea kule kujitoa na kujua kuwa ITS ALL ABOUT JESUS na wala hakuna kingine. Kumpa Mungu muda wake, kumfanya MUNGU KWANZA, kumuonyesha heshima anayostahili, kumpa utukufu wake, kumuonyesha ile thamani ya upendo na mapenzi yakulemea. Naongelea ile nidhamu na bidi ya mwenye maarifa ambaye muda wake na Mungu ni wa thamani kuliko muda wake na mke wake au mpenzi wake au kampani yake kwa kiwango ambacho simu si kitu mbele za MUNGU. Kanisani atawahi, atazzima simu bila kutangaziwa kanisani maana anayo biblia mkononi mwake. Moyo wake umemwelekea Mungu ili Mungu ajidhihirishe kwake. Ni nini naweza kutoa kwa ajili ya kudhihiridha upendo wangu kwa Mungu?

Upendo hauna kulazimishana. Upendo hauna kutumia nguvu ili jambo lifanyike. Upendo hauna mabavu. Upendo hauna kukwepa. Kwani ni mpaka watangaze maombi kanisani au kwenye huduma ndipo mtu aombe? Huu ni ulemavu mbaya sana. Kama kuna sababu ya kutupunguzia bidii yetu kwa Mungu basi ni upendo. Kama ni upendo basi kuna mambo yanahusika sana katika kutuhamisha upendo wetu kwenda kwenye vitu vingine.

WE LOVE GOD BY OBEYING.

YKM: Fulfilled In Jesus, Satisfied In Christ

Raphael JL
+255 767033300
Dodoma, Tanzania

Insta: @raphaellyela
Youtube: Raphael JL
Web: www.ykm.or.tz
Www.fichuka.blogspot.com

Maoni 1 :

Inaendeshwa na Blogger.