Ads Top

UMUHIMU WA BIDII KATIKA KUMTAFUTA MUNGU.


UMUHIMU WA BIDII KATIKA KUMTAFUTA MUNGU
Bidii na juhudi zinahitaji maarifa sahihi kumsidia mtu kupata anachotafuta kama anatafuta mahali sahihi. Mfano, ukipoteza funguo, unaweza ukaitafuta kwa bidi na juhudu, yaani kwa nguvu zako zote kila mahali na usiione. Hii ni kwasababu unakuwa umekosa maarifa ya kujua huwezi kuitafuta kila mahali kabla hujaanza kuitafuta mahali ulipoipoteza. Ndo maana watu hupita njia ile ile aliyopita kabla hajapoteza mathalani anaweza kuikuta njiani. Kwa Mungu ni zaidi sana kwani yeye mwenyewe ameshasema anawapenda wampendao na wale WAMTAFUTAO KWA BIDII WATAMUONA. Lakini pia amesema katika Warumi 10:2 umuhimu wa kumtafuta Mungu ukiwa na maarifa au ufahamu. Yote mawili ni muhimu.

Dunia tuliyopo ina mambo mengi sana ambayo YANAFYONZA ile bidi yetu ya kumtafuta Mungu na badala yake tunajikuta tumechoshwa na vitu hivo. Ni vigumu kukubali ukweli ingawa pia ni aibu kuonekana UMEFONZWA nguvu na shauku yako kwa Mungu. Mambo ya Mungu yanapewa nafasi ya pili na mambo mengine ya maisha yanayoonekana kuwa na maana zaidi yako msitari wa mbele. Ni kama Bwana Yesu aliona na kuonya kwenye Mathayo 6:33 kuhusu kutoa kipaumbele kwa UFALME WA MUNGU kwanza. Lakini mazingira yakoje leo? Watu wanachukia kuambiwa wasome biblia kwa bidii. Wanaona wanahukumiwa wakiambiwa waongeze bidii ya kumtafuta Mungu.

Huwezi kukubali hili mpaka uwe mkweli sana na uangalie muda unaotumia kwenye MITANDAO YA KIJAMII kama WhatsaPP, Instagram, facebook, Twitter na mingineyo mingi tu. Muda unaotumia kuangalia sinema na picha za kihindi na za kichina na movie, sembuse zile za Kifilipino? Muda unaotumia kufanya hayo yote, linganisha na muda unaotumia kuomba, kusoma na kutafakari NENO LA UZIMA, kuutafuta uso wa MUNGU juu ya mambo kadhaa, kutumika na maeneo mengine ya maisha yako. Wakati unajipima jikumbushe pia ule moto uliokuwa nao pindi t undo umeokoka, ile shauku na ile bidi ambayo hakuna mtu angekukukatisha tamaa. Angalia leo, unaweza ukajikuta umebaki kujisifia tabia nzuri uliyokuwa nayo miaka kumi ilopita lakini sasa una kwashakoo ya kiroho. Umebaki na uhenga wa kuokoka miaka 30 ilopita. KUPOTEA RAHA HASA IKIWA MCHANA, USIJISIFIE KUPOTEA USIKU.
Ukianza maombi unasinzia baada ya dakika tano, ukiimba unachangamka. Ukianza kusoma neno la Mungu unapoteza channel baada ya dakika nne ila ukianza kupiga stori na kuangalia movie afya ya roho na mwili inarudi ghafla na unajikuta umelala saa nane usiku. Ibada ikipitiliza hata kwa dakika tano unachukia, unamchukia aliyechelewesha, unahama kanisa na kulilaani hilo kanisa milele, ila ukichelewa kurudi nyumbani kwakuwa ulienda kula dinner haina shida.

Hali ni kama ile ile tu, uimbaji wa kwaya dakika 50, matangazo lisaa limoja na neno la Mungu halitakiwi kuzidi nusu saa. Ukirogwa ukazidisha muda wa mahubiri sio tu kwamba watu watakuwa wameshasinzia bali watu wanaanza mgomo baridi wa kutokujibu kitu. Unashangaa nini sasa? Kama mama ni kanisa, fellowship za vyuoni zitakuwa na utofauti wa kiasi gani. Unaenda ibadani kwa maamuzi yako, unafika na kufurahia na kurukaruka sana wakati wa uimbaji na muziki. Neno linapoanza unapata dharula ya kutoka nje, unaenda unapunga upepo huku ukituma picha ulizopiga wakati wa PRAISE AND WORSHIP. Unataka umlaumu Shetani, tumuhurumie jamani.

Bila kuweka mikakati ya kuamua kubeba msalaba wako na kumfuata Yesu, bado NJIA ILE NI NYEMBAMBA SANA. Bidi yetu iko wapi? Daniel alisali mara tatu kwa siku, Daudi alikuwa anamsifu Mungu mara saba kwa siku, halafu sisi tuko tunajitia moyo kuwa USINIGUSE MIMI NI MBONI YA JICHO LA MUNGU? Daud aseme nini, Daniel asemeje? Bidii ya mambo ya Mungu inapingwa kila siku. Kila saa. Upendo unaodhihirishwa wakati wa kuimba tu ni upendo wa namna gani? Kumlingana Bwana ni gharama ya kiasi gani? ANYWAY. NAJIKEMEA. Yafikiri haya kwa kina, jipime na uamue leo. Ama sivyo utaendelea kuamini kuwa ipo siku mambo yatabadilika au utaendelea kuwa mlemavu wa kusubiria MAFUNUO YANAYOFUNIKA YA MANABII WA LEO AMBAO UJINGA,UVIVU NA UZEMBE WAKO NI FAIDA YA JUU KWENYE BIASHARA ZAO. POKEA NA HILI PIA.

AMANI YA YESU KRISTO IWE PAMOJA NAWE.


YKM: Fulfilled In Jesus, Satisfied In Christ

Raphael JL
+255 78710003
Dodoma, Tanzania

Insta: @raphaellyela
Youtube: Raphael JL
Web: www.ykm.or.tz
Www.fichuka.blogspot.com

Maoni 1 :

  1. Nmependa mafundisho yako nataman sana bidii na passion ya kumtafuta Mungu iwepo!!!! Be blessed pastor

    JibuFuta

Inaendeshwa na Blogger.