HUWEZI KUPIMA KAMA HUNA KIPIMO.
HUWEZI KUPIMA KAMA HUNA VIPIMO
Truth Point
Ni vigumu sana. Ni kama kusema pasipo maono huwezi kujizuia. Kama nguvu ya kujizuia inatokana na kuwa na maono halafu wewe huna maono, yaani huna ile nguvu ya kujizuia, ni wazi kuwa huwezi kujizuia. Kama hujui vipimo huwezi kupima lolote au chochote. Kama hujui halafu ukawa na bidii ya kufanya huwezi kupatia unachofanya kwani *bidii haibadilishi matokeo ya nafasi ya ufahamu au bidii haiwezi kuwa mbadala wa ufahamu.* Kukimbia spidi kwenye mwelekeo usio sahihi hakuwezi kukusaidia kubadilisha mwelekeo. *Katika bidii, maarifa ni nguzo.* Hutakiwi kuwa na kimoja na kukosa kingine. Vyote ni muhimu na vya lazima kila wakati.
Sasa wewe unadhani utapimaje na huna vipimo? Utasinziaje na hujalala? Utafikiaje mia na huna au hujaanza hata moja? Unataka kupima matokeo lazima ujue vipimo. Kama vipimo ni viwango sawa ila huwezi kupima kama hujui vipimo.
YKM: Fulfilled In Jesus, Satisfied In Christ
Raphael JL
+255 76733300
Dodoma, Tanzania
Insta: @raphaellyela
Youtube: Raphael JL
Web: www.ykm.or.tz
Www.fichuka.blogspot.com
Hakuna maoni: