Ads Top

MAOMBI YANAYOJIBIWA NIMETIBITISHA.


MAOMBI YANAYOJIBIWA, NIMETHIBITISHA!
Unataka maombi yako yajibiwe? Hakuna muujiza. Ni kuzijua na kufuata kanuni zilizopo, kwa sehemu nimeweza kuzipata na kuziona hizi hapa zinaweza kukusaidia:
1. Mungu hayasikii maombi ya mwenye dhambi
2. Kubali kujazwa nguvu za Roho Mtakatifu,
3. Tafuta mapenzi ya Mungu katika kila unaloomba, Mapenzi yake yatimizwe
4. Omba sawasawa na Neno lake, usitoe KAFARA YA WAPUMBAVU (Mhubiri 5)
5. Uwe na imani na omba kwa imani, HAKIKA YA BAYANA
6. Funga na kuomba, kuna mambo hayaendi bila kufunga na kuomba.
7. Endelea kuomba, omba bila kukoma. Mfano, Daniel aliomba mara tatu kwa siku.
Usichoke wala usiache mpaka imetokea. Elia aliomba mara saba kuirudisha mvua aliyoifunga kwa neno lake kama nabii wa kweli wa Mungu. Vipi mimi na wewe? Unaombea jambo unaishia njiani, chakula hakiivi, unakula kibichi, tumbo litakusumbua sana. Kubali kulipa gharama ya kuivisha chakula. Usiishie njiani. Omba mpaka ujue mapenzi halisi ya Mungu ni nini. Acha kujihurumia. Acha uzembe na uoga. Hata wale unaowafuata wakutabirie kama kweli ni watu wa Mungu wanafuata kanuni hizo hizo.

YKM: Fulfilled In Jesus, Satisfied In Christ
Raphael JL
+255 76733300
Dodoma, Tanzania
Insta: @raphaellyela
Youtube: Raphael JL
Web: www.ykm.or.tz
Www.fichuka.blogspot.com

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.