Ads Top

UMUHIMU WA MAHUSIANO KATIKA MAISHA YA KIJANA.


THE YARDSTICK OF TRUTH
Umuhimu wa mahusiano katika maisha ya kijana
Kama wewe ni kijana na hauko wala hujawahi kuwa kwenye urafiki wenye mahusiano yenye lengo la kuwafikisha kwenye ndoa basi soma kwa makini. Kama wewe ni kijana na uko kwenye mahusiano hivi unavyosoma basi soma kwa bidii ya moyo. Kama ulikuwa kwenye mahusiano au upon a mambo hayaendi vizuri au na kwasababu hiyo huoni haja tena basi rudia kusoma mara kadhaa. Uchaguzi ni wako wewe. Unaweza kupuuzia na kudharau lakini bado kuchanganyikiwa kuko pale pale. Ni vema kutoa umakini kwenye maeneo ambayo yanaathiri sana maisha yetu kila siku kwa kiwango cha hata kuondoa utulivu na ufanisi katika utendaji.

Kuna watu hawali hata chakula, wengine hawana furaha hata kidogo na wengine hawaoni sababu ya kuendelea kuishi. Wengine wameamua kuwa wahuni tu kama vile kulipiza kisasi, yaani kumkomoa adui kwa kuacha mlango wazi. Wengine kila siku ni kulia na kuliza au kulizwa na kulizana. Kuwa na rafiki, kuwa na mpenzi. Wengine wako kwenye uchumba ambao wanajua kabisa mioyoni mwao kuwa umelazimishiwa ila wanaogopa watu watasemaje kama wakiachana leo, wengine wamkuwa wapenzi kwa miaka 10 na bado sio wachumba na hawaelewi kwanini hawaelewi wanachopaswa kuelewa. Ukweli inaumiza sana. Kuna yale maumivu ambayo unaweza ukayapata mpaka ukajisikia kucheka kwa maumivu.

Ukweli unasemwa wapi? Labda ni maeneo machache lakini lazima kuna mahali unasemwa. Angalia sasa, kazini unaharibu kazi ulizopewa, furaha yako imeondolewa na jambo ambalo ulidhani lingekupa furaha na amani. Hucheki tena kama zamani. Tabasamu imefukiwa na machozi ya moyo. Unatamani kutoka unashindwa na vyote vinakuliza, unalia kuachana nae na unalia pia kubaki kwani ni kama hali halisi unaijua. Umejifunza na kufundishwa mengi. Umesoma vitabu na kuangalia movie na kusikiliza watu wanaofundisha lakini bado hujapata kile kitu cha kweli. Hutaki kusema ukweli mpaka ukweli ubaki kuwa kitu pekee cha kusema. Unaishi ndani ya mahusiano kwa mawazo ya watu.

Angalia ulikotoka, kabla hujawa na mpenzi na kabla hujawa na ndoto maisha yalikuwaje. Usikimbie wala usiache. Huwezi kubaki mtoto milele na wala hutakaa uzeeni milele. Ni lazima uvuke toka hatua moja kwenda ingine. Unavukaje sasa? Uliyemvisha pete, moyoni mwako hana nafasi kama ambaye ulitaka kumvisha kwakuwa ulimpenda. Ni kweli ana pete yako na wewe una pete yake ila huna moyo wake. Ila unaendelea tu mbele ukiamini utajifunza kumpenda. Kumbuka kujifunza sio jambo jepesi, lina gharama kubwa tu. Kwanini usijifunze leo? Wewe huelewi kama ambavyo yeye pia  haelewi kwanini mko hapo. Hamsongi mbele wala hamrudi nyuma ila mnaamini kuna mahali mnaenda. Hamshibi wala hamuoni njaa ila mnaamini mnakula.

Angalia vizuri. Ukiwa kwenye mahusiano yasiyo sahihi hakuna utoshelevu unaupata kwani utoshelevu umefichwa ndani ya usahihi. Basi leo angalia na uchague aina gani ya machozi. Petro alitembea juu ya maji kwa imani, wewe unachaguaje? Alitembea muda mrefu? Hapana. Alifika mahali akaogopa, akapata wasiwasi na mashaka. Akamwita Yesu amsaidie na ikawa hivo. Na wewe muite na uwe mkweli kwamba unataka msaada. Kuwa muwazi na mkweli. Yote yanaweza kukumiza, yaani kubaki au kutoka lakini huwezi kuwa kwenye yote kwa wakati mmoja. Haya mambo yameharibu vipawa na huduma za vijana na hata mpaka sasa.


YKM: Fulfilled In Jesus, Satisfied In Christ

Raphael JL
+255 767033300
Dodoma, Tanzania

Insta: @raphaellyela
Youtube: Raphael JL
Web: www.ykm.or.tz
Www.fichuka.blogspot.com

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.