USILAZIMISHE AKUKUBALI KAMA HAJAKUBALI.
Truth Point.
Unavuta kamba ili akupende unavyompenda? Upekee unakataa na utofauti unapinga. Kama hakuelewi sasa, mpe muda. Anaweza kuja kukuelewa akiwa anaishi na kosa lake huko mbele ya safari. Usimlazimishe. Usimsukume. *Usimtengenezee mazingira mpaka na yeye akiri kwa kinywa chake kuwa anakupenda.* Usimlazimishe akukubali. Je, kama anayo sababu ya msingi? Usibomoe mlango wakati umekuta chumba kimefungwa na kufuri. Sio kwamba waliofunga wamekosea. Ipo funguo. Ukifanikiwa kumlazimisha akuelewe au akuoe au muoane au akukubali ujue umejitakia lawama zile zile za kucheka mbele ya kioo.
Kuna vitu haviwezi kubadilika ndani ya wale tunaotamani wabadilike hata leo. Tunataka wawe kama sisi. Waimbe kama sisi. Waongee kama sisi. Wawe wanapiga miayo kama sisi. Wawe wanaamka OFF MOODS kama sisi. Fahamu hivi, *kuna vitu havitakuja kubadilika kwao na hasa kama wao wenyewe hawajamua.*
Unatumia nguvu kiasi gani kumshawishi auone upendo wako na jitihada zako? Umefanya mara ngapi mpaka sasa?
Labda umetumia nguvu zako sana. *Acha Yesu akusaidie sasa.* Kaa pembeni. Kubali umeshindwa. Akili zako zimepelea. Hii ni njema zaidi kuliko kuendelea kusukuma mpaka unaingia whatsapp na unaangalia kama ujumbe wako umesomwa, unagundua amesoma kabisa halafu unabaki na maswali mengi ambayo huwezi kupata majibu yake. Ni vema uwe muangalifu ili unapomkimbia adui A usijikute umekimbilia kwenye nyumba ya adui B na ukamkuta ameshika picha yako mkononi.
YKM: Fulfilled In Jesus, Satisfied In Christ
Raphael JL
+255 76733300
Dodoma, Tanzania
Insta: @raphaellyela
Youtube: Raphael JL
Web: www.ykm.or.tz
Www.fichuka.blogspot.com
Nakuelewa sana Ps Raphael
JibuFuta