WEWE NI MWEPESI SANA KWAKWELI.
WEWE NI MWEPESI SANA KWAKWELI.
Wewe ni mwepesi kama husamehi waliokukosea. Wewe ni mwepesi kama unawinda wake au waume za watu. Wewe ni mwepesi kama umeufanya mwili wako kama mdoli wa kuchezewa na kila mtu. Wewe ni mwepesi kama kila ukionywa unasema umehukumiwa. Wewe ni mwepesi kama unafanya vitu kwa kuiga,ANGALIA USIJE IGA KUPUMUA. Wewe ni mwepesi kama unaishi maisha ya kujilinganisha na wengine. Wewe ni mwepesi kama hujui moyo una nguvu kuliko mkono. Wewe ni mwepesi sana kama unajidharau na kujiona hufai. Wewe ni mwepesi kama ulimwamini aliekwambia huwezi. Wewe ni mwepesi kama unaishi kwa MOODS. Wewe ni mwepesi kama ukiambiwa ukweli unanuna na kuvunja urafiki. Wewe ni mwepesi kama unajichubua ili ngozi yako iwe kama ya Michael Jackson. Wewe ni mwepesi kama unataka kuitwa Rihana na huku wewe ni Uyanjo. Wewe ni mwepesi kama unajua unatakiwa kubadilika lakini unatetea ujinga wako.
YKM:Satisfied in Jesus
Iko vizuri
JibuFuta