Ads Top

GOD INCIDENCE YOUTH CAMP : UFALME WA MBINGUNI Mwl Makwaya:



Mathayo 13
Mathayo 6:9

“Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe,Ufalme wako uje.
Kuwa na Mahusiano na Baba
  Yohana
Kumsifu Baba, due to the relationship
Ufalme unajumlisha mfalme na pamoja na milki yake.
Ukimuua mfalme unakuwa umeuchukua Ufalme.
Zipo falme mbili ambazo tunauchaguzi wa kuamua kuchagua moja.
Unapokuwa chini ya Ufalme huna budi kufanya atakavyo mfalme wako. Mathayo 6:10a
Mfalme anawajibu wa kuhakikisha usalama na ulinzi kwa watu wake.
   Mathayo 6:13b
   Zaburi 121:4-5

Mfalme anawajibu na kuhakikisha watu wake hawafi njaa.
Mali na miliki zote humilikiwa na mfalme, raia huwa wanauwezo wa kuzitumia.
   Mathayo 4:1-4
   Muhubiri 12:1
Mathayo13:24-52

Moja ya sifa za mwalimu mzuri ni pamoja na aina ya mifano anayotoa kwa wanafunzi wake
Hivyo tunasoma sehemu nyingi sana Yesu anaongea/anafundisha kwa mifano.
Na ili uelewe kinachokusudiwa kwenye mfano ni muhimu kujua kinachohusishwa kwenye mfano.
Mathayo anaonyesha Yesu wakati anatoa mifano ya Ufalme wa mbinguni katika sura ya 13 mitatu alikiwa na makutano mitatu yeye na wanafunzi wake.
Anatoa mifano sita kuhusu ufalme wa mbinguni.
Tuigawanye mifano hiyo katika makundi 3;
Uthamani wa ufalme wa mbinguni ili tuupe kipaumbele........ (thamani)
Athari ya Ufalme wa mbinguni ndani yetu kwa wengine ........(Athari-Dare to impact)
Kutosumbuliwa na falme nyingine sababu kuna siku ya kutofautishwa....... (Matokeo)

UTHAMANI

UFALME WA MBINGUNI UMEFANANA NA HAZINA NA LULU)

Kitu chochote chenye thamani kwako utakitunza.
Na vitu vyenye thamani huwa vinalindwa.
Thamani: Gharama au ubora wa kitu kutokana na hali na kuhitajika kwake na jamii, bei.
Kitu chochote usichokijua gharama au ubora wake ni rahisi san akukipuuzia au kutokichukulia maanani.
Ukiijua thamani ya ufalme utajua jinsi ya kuitunza.

HAZINA

“Tena ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika shamba; ambayo mtu alipoiona, aliificha; na kwa furaha yake akaenda akauza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile.”
 Mathayo 13:44
Hazina haiwekwi upembuni wala hadharani, hazina hufichwa pasipofikika kirahisi ingawa unaweza kuwa unapita kila siku na usijue kuwa unapita katikati au juu ya hazina .
Kusitirika kwake haimaanishi kuwa haupo
Sasa Yesu anasema hazina iliyositirika na mtu mmoja akajua kwamba kuna hazina imesitirika katika shamba la mtu.
Uthamani wa hazina hiyo alienda kuuza kila alichonacho na kulinunua shamba hilo, ila sababu ya kuuza alivyonavyo haikuwa shamba bali hazina ndani ya shamba.
Hivyo kama huwezi kujitoa kwa vyote ulivyonavyo kwa ajili ya ufalme wa mbinguni basi hujui uthamani wa Ufalme wa mbinguni.
Marko 12:30
            Tunatakiwa kumpenda Mungu:
  •          Kwa moyo
  •           Kwa roho
  •         Kwa akili
  •         Kwa nguvu.
Mathayo 11:12

: Hazina

 Mali au vitu vya thamani vilivyohifadhiwa pazuri
Mahali ambapo shughul za serikali zihusuzo fedha zinaendeshwa.
Tuna maana mbili za kuziangalia;
Mahali- eneo (Moyo)
Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake”
         Luka 6:45
         Mithali 4:23
         Zaburi 19:14

Mali au vitu- Vinavyoshikika.
Moyo unatabia ya kufuata hazina ilipo.
Kuna watu wanamfuata Mungu sio sababu wanampenda bali sababu kuna vitu.
sasa uzuri Mungu alilijua hilo akaweka utaratibu Mathayo. 6:33

Lulu

“Tena ufalme wa mbinguni umefanana na mfanya biashara, mwenye kutafuta lulu nzuri; naye alipoona lulu moja ya Thamani kubwa,
alikwenda akauza alivyo navyo vyote, akainunua” Mathayo 13:45-46
                                                        Mwl Makwaya:

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.