Ads Top

GOD INCIDENCE YOUTH CAMP:FAIDA YA VIJANA WALIOTENGENEZWA KWA KANISA NA TAIFA


Mithali 29:18.
  Pasipo maona, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu Yule aishikaye sheria.
Kama una maono na hauna vitu unavyojizuia basi bado hujafuzu.
Sehemu ya kwanza ya kujizuia ni kujua nani wa kuambatana nae
Ukiondoa praise and worship makanisani. Vijana hawana faida tena makanisani.
Chochote kinachotengenenzwa kinatengenezwa kwa sababu.
Kutokujua sababu hakimaanishi hakina
Sababu (nia) huanzia kabla ya kutengeneza jambo
Nia ,Sababu , Lengo
Nia, huanza kabla ya kutengeneza jambo.
,mwanzo 1:26
Sababu huanza kabla ya kutengeneza kitu inapojulikana, ndipo swali tunatengenezaje hufuata
Namna ya utengenezaji itaamua kufkiwa kkwa lengo kwa kiasi hani au kutokufakiwa kabisa
Na kila kutengeneza kuwe kizuri au kubaya kuna sababu (nia) yake inayompa nguvu mtengenezaji.
Unaopokomaa kujua nia, pia ujue na njia
Yohana 4:
Utengenezaji unaohusisha na kuchukua muda mwingi, akili nyingi, pesa nyingi, watu wengi, huwa unaitwa uwekezaji
Katika uwekezaji tukipatia kuwekeza tutafaidika sana, ni kuwekeza ndani ya watu wetu wenyewe haswa kwa watoto na vijana”  Kila kitu kinatengenezwa.

KWANINI VIJANA:

  • Wana nguvu- Mithali 20:29, 1 Yohana 2:14
  • Wanaangalia zaidi mbele- Yohana 21:18
  • Ni rahisi kufundishika
  • Ni wepesi wa kuthubutu (risk taker)
  • Wanatengeneza kuishi miaka mingi mbele.
Sababu hizo zinatosha kabisa kuuonesha ni kwanini tuwekeze au tutengeneze vijana kwa faida ya kanisa na taifa.
Tunawatengenezaje vijana?
Ikumbukwe ndio kundi linakutana na changamoto  nyingi kuliko kundi lingine lolote.
Wazee wengi hata viongozi wengi wameshalikatia tama kundi hili.
1Timotheo 4:11
Kudharaulika au kuheshimika kwa kijana,  Kuko ndani ya kijana mwenyewe.
Vijana wanadharauliwa kwasababu;
Usemi na mwenendo.
Adolf  Hitle aliwah kusema “He alone, who owns the youth, gains the future”

FAMILIA, KANISA NA SERIKALI.

Eneo la kwanza kabisa kijana huanza kuandaliwa kuwa alivyo ni familia.
Familia- tabia na uvumbuzi wa vipaji
Eneo la pili ambalo kijana hupaswa kuandaliwa na kujengwa ni kanisani.

MAENEO 3 YANAYOMUANDAA KIJANA

  • Familia
  • Kanisa
  • Serikali

FAMILIA NA KANISA

Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye  hata iacha hata atakapokuwa mzee. Mithali 22:6
Wakawa wakidumu  katika fundisho la mitume, na katika ushirika na katika kuumega mkate, na katika kusali. Matendo 2:42

            MAANA ZA MANENO YA MSINGI

Lea:
Tunza Na Fundisha Mtoto mpaka Akue; Elimisha, Funda, Funza
Tunza:  weka chini ya uangalizi ili kisiharibike au kisidhurike
Fundisha: toa mafunzo elimisha, somesha,
Neno LEA lilitumika kwenye mithali 22:6 katika biblia ya KJV wametumia neon TRAIN
Train: Teach (a person or animal) a particular skill or type of behavior through sustained practice and instruction. (theory and practical)

      KULEA KATIKA NJIA IPASAYO

Kuwajulisha vijana Mungu wa kweli.
 2Timotheo 1:1-6
Ni kazi ya mzazi kumjulisha motto Mungu wa kweli
Kama ni kanisa ni kazi yetu kuihubiri injili na watu wanapompokea Kristo wanafanyika kuwa watoto. Yohana 1:12
Hatuwezi kumjulisha mtu kitu ambacho na sisi hatukijui. Ndio sababu badala ua kujaza waumini na wanachama kanisani tujazw wanafunzi wa Yesu. Hosea 4:9
Msaidie kulijua kusudi la kuzaliwa kwake.
Luka 1:13-17
Waamuzi 13:8

Kwenye kila changamoto inayolipata kanisa au taifa kuna mtoto/kijana alizaliwa kuondoa changamoto hiyo.
Mathayo 11:1
Ni kazi ya wazazi na kanisa kumsaidia kijana kujua kwanini alizaliwa
Watu wengi ndani ya kanisa na taifa kwa kuwa hawajui kwanini wapo, mchanganyiko wa utendaji lazima ulitese kanisa.
Kwanini ulizaliwa?

Msaidie kupata elimu

Mfumo wa kanisa unatakiwa uwe na namna ya kutoa elimu (mafundishi- mafunzo) zaidi ya Mahubiri.
Kufundisha
Kuhubiri
Kuponya
Mathayo 4:23; 9:35, Matendo 1:1;4:2, 5:42; 15:35

Mfundishe kufanya kazi. 

1 Samweli 3:1
Tuna kizazi cha watu wavivu sababu tangu nyumbani hakifundishwi kufanya kazi.
Mbaya zaidi hata shule za siku hizi nazo hazimfundishi motto kufanya kazi
Kama Mungu yeye anafanya kazi basiinapaswa kuanza kufundishwa tangu mtu akiwa mdogo kabisa.
Kazi ni wajibu.
Kazi ni ubinadamu.
Kazi ni utu.


Mfundishe kufanya maamuzi.

 kumb 30:19
Maisha ni jumla ya maamuzi mengi unayofanya toka katika chaguzi lukuki zinazo kujia mbele yako kila siku.
Maamuzi mazuri na sahihi huambatana na kujua kuweka vipaumbele na kuviishi.
Kama siwezi kusimamia kile nilicho amua basi wengine wataniamulia cha kusimamia.
Kumfundisha mtu namna ya kupambanua mambo ni moja ya njia nzuri ya kumfundisha kufanya maamuzi.
    Na Mwalimu  EMMANUEL  MAKWAYA
                              

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.