Ads Top

NGUVU YA UWEPO:NGUVU NA THAMANI YA MTU MMOJA



TUTASIMAMIA MWANZO 3:9

Swala na swali la uwepo wako mahali popote pale hata ndank ya Kingdom Ladies ni swala na swali la nafasi yako.
 *MUNGU ALIMUULIZA ADAM.....UKO WAPI?* maana yake uwepo wako hauonekani kwenye ile nafasi yako.Umehama.

Moja kati ya vitu vibaya kukutokea ni kukaa nje ya nafasi yako, kwani kukaa nje ya nafasi yako ndio tiketi rahisi ya kufanya uwepo wako usiwe na nguvu wala maana.

Kama Adam wa kiume aliulizwa....uko wapi?.ina kuna nafasi alikuwepo na akatoka...alipotoka kwenye nafasi yake tu na uwepo wake ukapotea.

 *_NOTE: Uwepo wako unatafsiriwa kwa nafasi yako.usipojua nafasi yako wala usijigambe kwamba uwepo wako una lolote la maana.*

Uwepo _ presence is the function of nafasi_ position.Uwepo wako una nguvu sana kama unajua nguvu na maana ya uwepo wako mwenyewe.ndo maana kuna watu hata wakiondoka kanisani au fellowship au home wala watu hawakukumbuki mpaka unarudi na kujitambulisha  ndo wanashangaa loh umerudi? Kumbe hukuwepo?

Ukiwa na rafiki ambaye hajui nafasi yake ujue uko na bomu ambalo limetegeshwa.ukigusa tu unalipuliwa.

Sio lazima kujulikana na watu wengi ila ni.muhimu kujulikana na watu ambao umejiunganisha nao.uwepo na nafasi yako ni mapacha wasioweza kutenganishwa hata kidogo.

 *KANUNI YA UWEPO INA MAMBO KADHAA YA KUYAJUA NA KUYAZINGATIA NA KUYAELEWA:*

1.LAZIMA UWEPO KIMWILI-YOU MUST BE PHYSICALLY PRESENT. Hii inamaanisha kuwa thamani ya uwepo wako lazima uwepo kimwili kwenye eneo husika ili uweze kunufaika  na mambo ya eneo hilo.ndio maana shuleni kuna kuita mahudhurio ili kujiridhisha kuwa mtu yupo kimwili na sio kiroho.  Kwenye kanuni za kujifunza lazima mwili wako uwe hapo. Huwezi kuituma roho yake iende shule na mwili wako upo sehemu nyingine.
Uwepo wako sehemu ya kwanza ni mwili wako.
Kumbe hapa duniani wote waliopo wapo katika mwili, siku mwili wako haupo ujue umeshaondoka na hauna kazi wala maana yeyote kimwili.  Ukishakufa huna lolote la kufanya kimwili.
Kuwepo kimwili ndio tiketi pekee ya kuwepo duniani.
 *Yohana 1:14* ,
YES, NENO(YESU) ALIFANYIKA MWILI....yaani bila huu mchakato wa kuwepo kwa Yesu duniani katika mwili  kazi ya wokovu ingekuwa haitabiriki. Ilibidi afanyike mwili ili apate kibali cha kufanya kitu duniani.
Ngoja nikazie hapo usipojua namna ya kuutawala mwili utakosea makosa makubwa makubwa, na ndo maana waswahili wanasema fimbo ya mbali haiui nyoka.
Lazima mwili uwepo ili mengine yote yaweze kuwepo.
Roho nafsi vyote vimebebwa na mwili wako.hivyo utaona ni lazima mwili wako uwepo mahali husika ili uweze kufaidi  utukufu wa mahali hapo.

2.YOU CAN BE PRESENT PHYSICALLY BUT NOT AVAILABLE.
kuwepo kimwili mahali sio Alfa na Omega.yaani unaweza kuhudhuria kabisa semina au ukawepo kabisa kwenye group lakini ukawa hupatikani.unaweza ukawepo lakini ukawa hupatikani.kuna watu ni mabingwa kweli wa kuhudhuria semina na makongamano lakini ukiangalia na kiwango chao cha maisha na mahudhurio havifanani. Kuandika sio kupatikana.wengi wamejaza notebook ila kiwango cha Maisha yao ni kama chekechea.
PRESENCE AGAISNT AVAILABILITY.
Ni kweli upo ila unapatikana?
Kinachofanya mtu apatikane ni ushiriki wake wenye malengo katika jambo husika.
 KWA YOU MUST BE ACTIVE TO BE AVAILABE SOMEWHERE....
Ndo maana unabaki kushangaa mtu kaenda kanisani, wakati wa uimbaji yupo active neno likianza tu anaanza kusinzia dishi linahama.
NI HERI UWE GAIDI WA KISIASA KULIKO UJASIRI WA KUSINZIA WAKATI WA NENO....
Kama unajua kwanini upo kimwili basi lazima ujue kwamba usiposhiriki unakua butu na  unapoteza sifa za kwamba ulihudhuria.

3.YOU CAN BE AVAILABE BUT NOT CONNECTED.

Hapa maana yake upo kweli na unapatikana lakini hujui kwa nini upo, hali hyo ya kutokujua inakufanya unajiona out of space.usipojua kwanini upo mahali utapata tabu.
HAYO MAMBO MATATU YANATOSHA KUTUPA PICHA NZURI KUHUSU UWEPO WAKO.
Kama umeshaelewa kusudi la kundi ni kujipanga tu kuangalia ni jinsi gani utakuwa sehemu ya yanayoendelea badala ya kujitenga.ielewwke huwezi kufanikiwa pasipo na watu
Tunahitajiana kwa namna moja ama nyingine.usijidharau kwa kujiona hauna maana.

By Raphael JL
0767 033300
YouTube:Raphael JL
Instagram:Raphaellyela
www.fichuka.blogspot.com

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.