NAMNA AMBAVYO MAHUSIANO YANAATHIRI HATMA YA MAISHA YETU.
DESTINY-HATMA ni mwisho wa jambo,kwa tafisiri nyepesi na ya kawaida sana, bila kuyakuza mambo. Hatma ni mwisho wa mwelekeo wang au wako. Kila jambo lenye mwanzo lina hatma katika tamati yake. Hata kwenye mahusiano pia. Nini hatma ya mahusiano yako? Unaweza usijue nini hatma ila lazima ipo na hiyo hatma inaathiriwa na mambo kadhaa ambayo kwa sehemu ndio tunajifunza leo kwa kutumia kanuni tatu au zaidi kwa pamoja.
*Zipo kanuni zinaweza kukusaidia kuwa mahusiano mazuri na ya kufurahisha kama ukiamua.*
*_Kanuni ya Kwanza_ : _KANUNI YA USAHIHI._*
Hii ni kanuni kubwa sana kwenye mahusiano.usahihi ni maamuzi, yaani ukishajua uliye naye ni mtu sahihi unakuwa na ushindi wa asilimia 20 hivi.
KWENYE USAHIHI UNAJIULIZA MASWALI KADHAAAAA
1. WEWE NI SAHIHI KWAKE?
2.YEYE NI SAHIHI KWAKO?
Kikubwa cha kuelewa hapo ni kuwa usahihi umefungwa kwenye nani na sio nini.its all about WHO and not WHAT.lazima wote muwe sahihi japo asilimia 20 za usahihi haziondoi asilimia 80 za kuwajibika.
Ni rahisi sanaa kuishi na mtu asiye sahihi nakwambia.asilimia kubwa sana ya watu wasio sahihi huwa ni wakamilifu sanaa na pretenders wa kutupwa.
Watu wasio sahihi hujitahidi sana kukaa mahali sahihi lakini kwa kuwa wao sio sahihi jitihada zao huwa hazidumu kwa mtu mwenye uelewa.
Shauku yako ya kupatia haitakiwi kuzidi kusudi lako la kufanya, kuwa au kujua vinginevyo utajikuta umekosea zaidi ya kiu yako ya kupatia
Usahihi hauondoi changamoto au madhaifu
Kumpata mtu sahihi kwenye maisha yako ambaye ndo unaamini unaenda kuanza nae maisha ya ndoa hakuondoi changamoto za yatokanayo na nyie wawili.
Japo kwamba ni mtu sahihi lakini bado usahihi ni wa ule uchaguzi ulioufanya wa kumchagua yeye na sio wa kuondoa changamoto au udhaifu.
Wengi husahau kuwa ni kweli ni sahihi lakini bado ni mwanadamu, bado ana mapungufu,bado ana madhaifu ya kutosha tu, anaweza akawa sahihi na bado akawa mjinga, akawa mshamba, akawa sio wa kiroho kwa vipimo vyako lakini ni sahihi.
Hakuna mtu huwa anataka wala kutamani kukosea kwenye mipango na ndoto zake lakini,
Bahati mbaya sana ile hali ya kutaka kupatia sana hata kuwa tayari kutokujali kuhusu kusudi la jambo lenyewe husababisha ndani yetu mawazo, mchanganyiko kwa namna ambayo wengi hujikuta hawajui nini la kufanya lakini huamua kufanya ambalo linaleta ladha ya wakati kwa mihemko ya hofu au mashaka au wasiwasi.
Kupatia kuoa na kupatia kuolewa ili mpatie kuoana, lakini nataka muone upande wa pili wa shauku hii ambayo inaweza kukuharibu pia. Ni kama vile kusema,asali ni tamu lakini ukiila kwa kuzidi inaweza kukuharibu. Kazi ya Mungu inaweza kuharibu mahusiano yako na Mungu usipokuwa makini.
Usipojua hilo na usipojua namna ya kuishi na mtu sahihi lakini mwenye mapungufu unaweza ukajikuta hakuna mahusiano yanayokufaa maana cha ajabu kabisa utakuwa hujui shida iko wapi huku ukijihesabia haki kuwa wewe uko sahihi.
Usahihi wake uko kwenye hatma lakini sio kwenye maisha ya kila siku ambayo ndio unatakiwa ujifunze ili ujue kuwa usahihi hauondoi nafasi ya kujifunza ili uwe bora zaidi
Mungu anaweza kabisa kukuonyesha kuwa fulani yule ndo mumeo au mkeo lakini umbali wa kutoka kwenye kuonyeshwa mpaka kwenye uhalisia wa maisha halisi unaweza kukuvugura mpaka ukabaki huna hamu na mahusiano milele.
Hii ni kwasababu kuonyeshwa ni jambo moja, lakini pia Mungu huonyesha utukufu wa mwisho ila mchakato wa namna ya kuishi huwa unabaki mikononi mwako moyoni mwake Mungu.
Kuingia kwenye mahusiano na mtu sahihi ni moja ya changamoto kubwa sana kwenye mahusiano ya siku hizi maana ni kama vile usahihi wenyewe haujulikani.
JIULIZE MWENYEWE, NANI KAKUFUNDISHA USAHIHI?
NANI ALIKUFUNDISHA USAHIHI? NANI ALIKUFUNDISHA KUHUSU MAHUSIANO? NANI ALIKUFUNDISHA NAMNA YA KUPATA JIBU SAHIHI? UNA PICHA GANI YA NDOA YAKO? UNATAKA NINI NA UMEJUAJE UNATAKA UNACHOTAKA? INFORMATION.....NAWASAMEHE MAKUNGWI KADHAA KWENYE HILI.
*_Kanuni ya pili: KANUNI YA KUISHI NDANI AU KATIKA USAHIHI_*
Asilimia kubwa ya watu wanaishi katika hali ya kutokuwa sahihi na wanategemea watu sahihi.unatakiwa uishi katika level ya usahihi in a way mtu sahihi akikuona anaweza kukutambua.be honest to yourself.
Mfano: unategemea kwenda Sumbawanga.kujua unatakiwa kwenda Sumbawanga it's who part, nani unaenda nani? Njia unajua? It's how part.
Kuna vitu vingi usipojua kabla hujaingia kwenye ndoa unaweza kuacha ndoa usiku wa honeymoon.
Ukimkubali mtu maana yake ni mtu sahihi ina maana kwamba umekubaliana na madhaifu yake. Mfano ukipeleka jambo la kuoa nyumbani lazima muwe mmetengeneza oneness.in a way mnaweza kuwatengeneza wengine wakakubaliana na nyie. Ukishajitambua who are you mambo mengine yote unaweza kudeal nayo.
Sio mahusiano yote yanayovunjika hayakuwa sahihi mengine ni namna ya kushindwa kuishi katika usahihi.
*_Kanuni ya tatu: KANUNI CHA UKUSANYAJI,UPATIKANAJI NA MATUMIZI YA TAARIFA_*
We are living in information age.
Unaweza kukusanya taarifa sahihi ila namna unavyozitumia zikaleta athari kubwa.
Mahusiano mengi yanafunjika sababu ya tafsiri mbaya ya taarifa.
Nyie wawili ndio chanzo cha taarifa so hakikisheni mnazichuja vizuri.
Serikali yenyewe ina msemaji mkuu same applied kwenye mahusiano yenu.
Kiongozi ni kiongozi na msaidizi ni msaidizi. Lazima ujue jinsi ya kupokea taarifa na kuzimeng'enya.
Taarifa ni chanzo kizuri mno cha kuharibu mahusiano.
*_Kanuni ya nne_* : KANUNI YA KUJIANGALIA
KWENYE KIOO UKIWA UMEFUMBA MACHO.
Ili uweze kujiangalia ni lazima uweze kujitazama, fumbua macho.usijiangalie wakati macho yamefungwa.
Wazo la kanuni hii ni kuwa usijidanganye, usijitie moyo.
Huna cha kupoteza, huna cha kuficha kama umejikubali kwenye hayo mahusiano.
Tafuta taarifa. Hakikisha unafungua macho.
Jikague mwenyewe kwanza.be honest to yourself.
Kuwa accountable kwa kila unachofanya.chukua wajibu na wajibika.
*_Kanuni ya tano_* : KANUNI YA KUUAMINI UPEPO KATIKA SAFARI MOJA.
Sifa ya upepo hautabiriki, haupangiki na wakati wowote unaweza kubadili mwelekeo.
Kwa kusema haya namaanisha usimwamini mtu ambaye hana mwelekeo wa maisha, hana vision, hajui matumizi mazuri ya kile ambacho anacho.
Kutembea na mtu wa aina hii itakusababisha kutumia nguvu nyingi sanaa kuyalinda hayo mahusiano.
Ili kuwa na mahusiano mazuri lazima muwe na maono yanayofanana.
Msipokuwa na kuelewana ndo ile utaishi na mtu upepo. analala Leo hajui kesho atafanya nini.anasikia jambo mahali linambadili mwelekeo.
Kuendelea kukaa kwenye hayo mahusiano ni maamuzi pia.
Lazima mtembee katika kusudi linalofanana. Shikaneni mikono mtembee pamoja.make sure umemwamini mtu sahihi.
*_Kanuni ya sita:*_ KANUNI YA KUJIOGOPA KWA KUMUOGOPA ANAEKUOGOPA
*_Kanuni ya saba*_ : KANUNI YA KUKATAA UNAYOYATAKA KWA KUYAKUBALI.
Kwenye mahusiano lazima ujue unachotaka ili ikusaidie kupata unachotarajia ili kikija ambacho hukutarajia iwe ni kwasababu nyingine na sio wewe mwenyewe kutokujua unachotaka.unachotaka unaweza kuwa unachostahili kama ukipatia katika kuwa mkweli kwa unachotaka pia.
*_Kanuni ya nane_* : KANUNI CHA KUCHIMBA KISIMA SIKU UNA KIU.
Wazo la kuchimba kisima wakati una kiu.kiu ni uhitaji.ukichimba kisima wakati una kiu utachimba kisima kwa pressure na hata energy yako itatukuwa kubwa.
Kuchimba kisima wakati una kiu kunaweza kusababisha ukasahau mambo ya msingi.
Kuchimba kisima wakati una kiu ni reactive response ambayo most on ladies wanakuwa nayo wen comes to relation .dont rush into relation because there is price to pay.when you say yes there will be price to pay and vice versa.
When a man comes u must make sure your in the same response as his.dont rush.
Usitengenezewe wala usijitenge uhitaji.ukitengenezewa na ukitengeneza zote ni external.its should be internal.should comes from within you.
Knowing that when u agree to be in relation u agree with anything concerning him including his family, friends etc.
Wacha maturity and growth take you to relation.
Wacha kuparamia.utakuja paramia mtu kavaa koti la upupu.
Ukisoma mwanzo utaona Mungu ndo aliona uhitaji wa Adam kutaka msaidizi na wala sio uhitaji wa Adam.
Kuna aina fulani ya baraka huwezi kuzipata hadi uwe umekuwa.
*_Kanuni ya tisa_* : KANUNI YA KUMHURUMIA ANAEKUUMIZA KWAKUWA ANACHEKA ILI USIVUNJE AGANO LAKO.
Moja kati ya changamoto kwa Adam wa kike ni kujihurumia.kuogopa kumpoteza, kila kitu ni kuogopa na kujihurumia mpaka unakuta unaishi kama mkimbizi kwenye mahusiano ambayo ulikuwa unayaota kwa sababu unatarajia tu kuwa one day itakuwa sawa. Ambacho unaweza ukawa huelewi wewe Adam wa kike ni kuwa hofu yako ya kujihurumia inaweza kukusababisha ukazidi kukosea zaidi kila siku.unaogopa kumuumiza anaekuumiza kwa gharama ya wewe kuendelea kuwa mtumwa wa maumivu yake? Na ndio maana wengi wanasema Mungu ana majibu matatu.kazi kweli kweli.
UKIUMIA KWA KUJITAKIA USILIE. VUMILIA TU haha ha ahahahahah.
Ni aibu kubwa sana kumsinguzia shetani kosa ambalo ulishiriki kwa asilimia 75.unapata wapi ujasiri wa kusema shetani alijiinua? Hujui ndio tabia yake kujiinua na ndo maana Bwana alishamshusha?
*NB* *:
Kuishi na kosa ni mateso makubwa kuliko kuchelewa kuolewa.
Kuishi na kosa ni lile wazo la kuingia kwenye ndoa kwa sababu za kipuuzi.
Kupotea kuna raha yake haswa ukipotea mchana.raha ya kupotea ni kuendelea kupotea ukiamini bado kidogo utapata njia sahihi na kumbe suluhisho pekee ni kurudi ulipotoka na kuanza upya.
By Raphael JL
0767 033300
YouTube:Raphael JL
Instagram:Raphaellyela
www.fichuka.blogspot.com
Hakuna maoni: