ACHANA NA NDEGE WA KUFUGWA, TAFUTA TAI WENZAKO.
“Surround yourself with GENERALS, not FOOT SOLDIERS. Surround yourself with EAGLES, not DOMESTIC BIRDS. Unajishangaa kwanini uko hivo ulivo? Angalia wanaokuzunguka. By Raphael JL:
Mithali 13:20
Enenda pamoja na wenye hekima , nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu ataumia.
Ni wazi na ni kweli kuwa watu wanaotuzunguka wanatuathiri sana namna tunavyowaza na kuongea na hii inaenda mpaka kuathiri mitazamo yetu au MACHUJIO. Na biblia imeonyesha wazi kuwa ukienenda na wenye hekima basi na wewe utakuwa na hekima, kinyume chake pia ni sawa, yaani ukitembea na wapumbavu na wewe utaishia kuwa mpumbavvu. Uchaguzi ni wako. Ukiruhusu kuzungukwa na watu ambao ni waropokaji au watu ambao wanaongea sana kuliko uwezo wao wa kufikiri ni wazi kuwa punde na wewe utajikuta ni mropokaji. Kibaya ni kwamba hutajua kuwa tabia yako imeanza kubadilika mpaka umekutana na mtu au watu waliokuwa wanakufahamu ulivyokuwa hapo nyuma.
Ndo maana Mithali 1:10 inasema:
Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi, wewe usikubali.
Wenye dhambi ni watu, sio miti. Ni kampani, sio mawe. Wenye dhambi ni watu au marafiki ambao wanamzunguka mtu na ndani yao wana ushawishi wa uharibifu. Watu wanaokushauri kukosea bila kujali hatma ya maisha yako. Watu wanaokushauri kujiharibu bila kujali kulinda utu wako. Ukizungukwa na watu wa aina hii ni wazi kwamba mwisho wa siku utajikuta na wewe unaanza kufanya na kusema na kuwaza wanayowaza na utajikuta umeumia. Na ndio maana Wakorintho wa kwanza 15:33 inasema hivi:
Msidanganyike; mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.
Kumbe ni rahisi sana kudanganyika. Kudanganyika kwamba mazungumzo mabaya hayawezi kuharibu tabia njema. Lakini ni ukweli kuwa mazungumzo mabaya au mazuri yanatoka ndani ya moyo ulio mzuri au mbaya ndani ya mtu. Mazungumzo ni maneno, maneno ni matokeo ya mawazo na mawazo ni matokeo ya akiba ya moyoni. Yaani ukiwa unazungukwa na marafiki ambao kila siku wao wanaongea pumba tu, ni wazi kuwa na wewe utaanza kuzielewa pumba zao na ndio maana huwezi kumuona TAI ANATEMBEA NA NDEGE WA KUFUGWA. Ni wazi na itoshe kusema kuwa ukitembea na wenye hekima ni lazima utajikuta ile hekima inaanza kuonekana ndani ya mawazo, maneno na mwisho matendo yako. Ndo maana Mathayo 12:35 inasema hivi:
Mtu mwema katika akiba yake njema hutoa mema; na mtu mbaya katika akiba yake mbaya hutoa mabaya.
Kwa hiyo unaporuhusu kuzungukwa na watu waharibifu ni vizuri ukajua kuwa wao watakuharibu kuanzia ndani pia maana akiba iliyotunza ujinga haiwezi kutoa ufahamu. Akiba iliyotunza uongo haiwezi kuongea ukweli. Akiba iliyotunza uzushi haiwezi kuongea usahihi. Wewe jikague tu. Jaribu kujipima. Kila ulipobadili wale wanaokuzunguka ni nini kilitokea ndani ya maisha yako. Hata leo unaweza kuutumia ujumbe huu kujipima na kufanya tathmini uone. Angalia kama kweli unaridhika na hali ya maisha uliyonayo. Umeridhika na kiwango cha ufahamu unachokionyesha kila siku? Umeridhika kuwa mtu wa aina hiyo?
Ukitaka kuwa muongo usikae na watu wakweli. Ukitaka kufanya biashara usikae na watu wanaowaza kuajiriwa. Ukitaka kuajiriwa usikae na wajasiriamali maana wanaweza kukufanya uache kazi na kuona kazi yako sio muhimu kwani unatakiwa kujiajiri mwenyewe. Unataka kufanikiwa usikae na watu walioshindwa. Unataka kuendelea mbele usikae na watu waliokwama. YOU CAN'T GIVE WHAT YOU DON’T HAVE.
Unataka kuwa mwalimu, usikae sana na wanajeshi. Unataka kuwa mwanajeshi usikae sana na manesi. Watu wanaokuzunguka na wenye ushawishi kwako wanaweza kukubadilisha sana kama hujajitambua vya kutosha. Ndio maana kama hujajitambua ni vigumu sana kufanikiwa bila kushusha viwango. Unataka kuoa usikae na watu walioachika. Unataka kuingia kwenye mahusiano usikae sana na watu waliopigwa vibuti maana watakujaza yaliyowatokea. Uzoefu wa mtu mmoja haumaanishi na wengine pia watapitia hali hiyo. KANUNI INA NGUVU KULIKO UZOEFU. A PRRINCIPLE IS MORE POWERFUL THAN EXPERIENCE.
Ninachosema hapa ni rahisi sana. Tai ni tofauti na njiwa. Wanafanana kwamba wote ni ndege. Lakini ndani yao ni ndege wawili tofauti sana. Wote wana macho mawili lakini wanaona kwa namna tofauti. Kama wewe ni tai halafu umezungukwa na njiwa unaweza ukawa unaongea na hueleweki. Wewe hujui kuwa kutokueleweka kwako kunasababishwa na ukweli kwamba umezungukwa na watu wenye ufahamu wa njiwa na wewe ni tai. Ndio maana wakati mwingine unaweza kusema kitu watu wasikuelewe, haimaanishi ulilosema sio kweli ila umelisema kwa nani? Anyway. Itoshe kusema ukizungukwa na makomandoo ujue ufahamu wako utaanza kukaa kikomandoo.
Ujumbe wangu kwa vijana wote duniani katika kukumbuka siku ile nilipoachiliwa toka rohoni mpaka mwilini na kuzaliwa hapa duniani.
Raphael JL: Classified mindset
Hakuna maoni: