MOVE WITH MOVERS CAMP : MAMBO YATAKAYOTUSAIDIA KUTEMBEA NA MUNGU NA Mwl. MGISA MTEBE.
Amosi 3:3
Kupatana ina maana zaidi ya kukubaliana bali ina maana pia ya
kuwa na Roho Moja pamoja na mwendo unaofanana. Hivyo lazima tupatane katika
Roho moja na mwendo mmoja na Mungu ili tuondoke naye.
Kama Roho wa Mungu
anapokoa anaondoka[MOVE] huo ndio unapaswa kuwa mwondoko wetu pamoja na ROHO WA
MUNGU.
Wagalatia 5:25
“Kiwango cha ushindi
na mfanikio katika kile ambacho Mungu amemuita mtu kufanya kinategemea sana ufahamu na ujuzi [Knowledge and
Understaing] wa NAMNA Mungu anavyofanya kazi”
Mungu ana namna yake
ya kufanya kazi. Usijifunze namna Mungu anavyofanya kazi kazini bali jifunze kabla ya
kazi. Tunajifunza kuogelea kabla ya kuanza kuogelea. Tunajifunza kuzima
moto kabla ya moto unaopaswa kuzimwa kutokea.
Mfano wa Daudi:
Aliandaliwa kwa Vita
na kwa wito wake kabla hajaingia rasmi(full time) kwenye Wito wake.
Nidhamu ya Mfalme
Daudi wakati wa Vita
Wito wa Daudi
1.
Kuwaunganisha Israeli
2.
Kupiga maadui wa Israeli; Alikuwa mtu wa vita sana
3.
Kuandika Zaburi
Wito wa Daudi ulikuwa
katika perfect will of God lakini
wito wa Sauli ulikuwa permitted will of
God.
Sauli alipakwa mafuta
kwa Kikombe[Man made] wakati wafalme na manabii wengine wote walipakwa mafuta
kwa Pembe[God made]. Hapa ndipo maana kamili ya Perfect Will of God na Permitted
Will of God. Yote ni Mapenzi ya Mungu.
Huwezi kuficha asili
yako kama. Kama umejipa wito bado utafahamika tu kwa asili ya wito wako.
Hadithi ya wazazi waliokuwa na mtoto wakilima shamba. Mara Fisi akelekea pale
mtoto alipokuwepo walipokwenda wakakuta watoto wawili, baadae punda akaelekea
pale na wakawa watoto watatu. Waliwachukua watoto wote bila kujua wa kwao ni
yupi lakini katika Maadhimisho ya Siku ya kuzaliwa kwa mtoto wao waliweza
kumtambua mtoto wao kwani mtoto mmoja alionekana migombani na mwingine kwenye
mifupa lakini mtoto wao alibaki meza kuu kusherehekea.
Ushindi wa vita ya
Daudi na Wafilisti ulitegemea UMAKINI wa
1.
Kuwa mahali sahihi; Kuwa na uwezo wa kutambua pale Mungu
anapotaka kubadilisha mahali talipopaswa kuwa
2.
Kuwa na watu sahihi. Unatembea na nani?
3.
Kufanya kwa wakati sahihi
4.
Kufanya kazi kwa kasi
Katika Wito ulionao
lazima ujue watu unaopaswa kutumika nao na uwaweke katika madaraja.
Watu walio chini yako
lazima wawe na roho yako. Lazima wawe na wito kama ulio nao. Huduma isiwe ndani
ya huduma nyingine.
Kukua katika WITO.
“If you miss the right
level you listen wrongly”
Ukiokosa nafasi sahihi utasikia
vibaya.
Kiroho tunaongezeka
ngazi kwa kushuka chini.
NAMNA YA KUTHIBITISHA WITO WAKO
Ishara au viashiria
vya wito wa MTU
1.
Amani na Furaha ya moyoni(Peace and joy):
Mithali 10:22, Isaya 55:12, Filipi 4:4-7, Kolosai 3:15
Haiwekazekani Mungu akupe kitu ambacho kinakukosesha amani.
2.
Kupenda na kuridhika(Passion) kufanya jambo/kitu Fulani.
Passion ni msukumo wa ndani wa kupenda kufanya unachofanya
hata kama haulipwi. Unaweza kudiriki hata kulipa ili upate nafasi ya kufanya
hicho unachotaka kukifanya.
Kutoka 33:12-14, Mathayo 17:1-7, Zaburi 37:4, Zaburi 16:11
3.
Kutoa muda wa zaidi na ziada.
Kutoka 33:7-11, Mathayo 14:22-23, Marko 1:35, Yohana 8:1
4.
Uwezo mkubwa wa kazi hiyo(Ability)
Kutoka 31:1-5, Matendo 6:7-10
5.
Matokeo mazuri ya unachokifanya.
Yohana 5:31-36, Mathayo 11:3-5, Marko 16:15-20
6.
Wito Mungu inatajirisha[Baraka na Mafanikio]
Zaburi 1:1-3, Mithali 10:22, Mithali 17:8, Mithali 18:16,
Kumbukumbu 8:12-18, 28:47-48
“Mungu anafungua
milango ya rasilimali fedha (utajiri)
ili tumtumikie kwa furaha”
Wito wa Mungu kwa mtu akitumika kwa uaminifu unalipa zaidi.
Tunaweza kureplace taaluma sio wito
7.
Ushuhuda mzuri wa watu wengine. Watu wengine watakwambia.
Na hii ni kutokana na matokeo ya kazi.
Mathayo 18:16, Yohana 6:11-14. Yohana 3:1-2, Matendo 6:1-8
Hakuna maoni: