MOVE WITH MOVERS YOUTH CAMP : GROWING IN THE KNOWLEDGE OF GOD THROUGH CHRIST na APOSTLE SHEMEJI MELAYEKI
KWANINI KUMJUA MUNGU
KATIKA KRISTO
Waefeso 1:17 “Mungu wa
Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu awape ninyi roho ya hekima na ufunuo katika
kumjua yeye”
KUMJUA MUNGU
kunahitaji Hekima na Ufunuo wa kumjua. Kama kuna kufunua kuna maficho yanayoficha
ufahamu kumhusu Mungu
Mungu anafanuliwa kwa
sababu amefichwa. Kuna namna watu hawamwelewi Mungu. Na kama humjui Mungu
huwezi kuwa na uhusiano naye.
2 Petro 1:2 “Neema na
iwe kwenu na Amani iongezwe katika kumjua Mungu na Yesu Bwana wetu”
Neema na Amani inaongezwa kwa kadiri unavyopata ufahamu wa kumjua Mungu.
Unapomjua Mungu unafahamu Mungu anawazaje, anatendaje,n.k
Epignosis[Greek word]Ă RecognitionĂ Full discernment,
acknowledgement;
This means the Highest Knowledge about
somethings and not only just knowing.
2Petro 3:18 “Lakini
kuweni katika Neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu
Kristo”
2 Peter 1:3 “Kwa kuwa
uweza awake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa KUMJUA yeye aliyetuita kwa utukufu wake
na wema wake mwenyewe”
Kukirimiwa ni Kupewa
kitu bila gharama yoyote (Zawadi)
MWILI NA DAMU (UFUNUO)
Mathayo 16:13-20
“Basi Yesu akaenda
pande za Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake wakasema, Watu hunena Mwana
wa Adamu kuwa ni nani? Wakasema, wengine hunena u Yohana Mbatizaji,
wengine Eliya, Wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii. Akawaambia, Nanyi
mwaninena mimi kuwa nani. Simoni Petro akajibu akasema Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu
aliye hai. Yesu akajibu akamwambia Heri wewe Simoni Bar-yona; Kwa kuwa
mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni. Na
ninakwambia, wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu;
wala milango ya kuzimu haitalishinda”
Haiwezekani sana
kupata ufunuo wa Mungu bila kuwa na Roho wa Mungu
Juu ya MWAMBA huu inamaanisha JUU YA UFUNUO huu;
Aina za ufunuo kuhusu
Mungu
1.
Ufunuo wa roho
2.
Ufunuo wa Mwili na Damu
Mtu anaweza kuwa na ufunuo wa Mungu katika roho na
Ufunuo wa Mungu katika Mwili na Damu.
Ufunuo wenye uhakika kabisa juu ya Mungu ni ule utokanao na Roho wa Mungu.
Namna tunavyomjua
Mungu inaathiri kila kitu katika maisha yako, kihuduma, kielimu, kiuchumi, n.k
KUHUSU KUMJUA MUNGU
1.
Watu wengi sana wanafikiri Kumjua Mungu Ni
a.
Kuwa na mistari mingi ya Biblia kichwani
b.
Jinsi unavyokuwa na nidhamu nzuri katika matendo ya Ukristo
kama kuomba na kutoa Sadaka
c.
Kuepukana na ubaya na watu wabaya
2.
Sehemu kubwa ya uelewa wetu juu ya MUNGU HAUJAJENGWA KATIKA
KWELI ILIYO KATIKA KRISTO YESU, BALI…
a.
Filamu za Kikristo
b.
Shuhuda za uongo makanisani kwa mfano Watu waliotoka
kuzimu, watu wenye mapepo, shuhuda zilizokuzwa.
“Kitu chochote ambacho kinapewa sauti kubwa kuwa mwangalifu nacho”
c.
Mafundisho ya Hofu
“Mungu ni mtakatifu sana kiasi kwamba anaweza kutakasa”
d.
Mafundisho ya watu wenye nia Mbaya.
MJUE SANA MUNGU
Ayubu 22:21 “Mjue
sana Mungu, ili uwe na Amani; ndivyo mema yatakavyokujia”
a.
Mstari huu ni maarufu sio kwa sababu ya watu kutaka kumjua
Mungu lakini kutokana na mambo binafsi yanayotakiwa.
b.
Hii ni lawama na dongo analopewa Ayubu kutoka kwa Elifazi
c.
Watu wanasukumwa na selfish
desire to get peace and prosperity and not KNOWING GOD
AYUBU ALIAMINI MUNGU
NDIYE ANAYEMTAABISHA, Hii inaonesha kabisa kuwa hata Ayubu hakuwa anamjua Mungu
vizuri.
Ayubu 23:16-17
“Kwani Mungu ameufanya
moyo wangu kuzimia, Naye mwenyezi amenitaabisha”
Mtazamo wa watu wengi
wa zamani haukuwa katika kumjua Mungu kiuhalisia, ndiyo maana sehemu nyingi
mabaya na mema yote walijua kuwa ni Mungu amewapatia
Ayubu 19:6-11
“Jueni basi kuwa Mungu
amenipotosha, Na kunizingira kwa wavu
wake. Tazama nalia, udhalimu, lakini sisikiwi, Naulilia msaada, wala hapana
hukumu. Yeye ameiziba njia yangu nisipate kupita, Na kutia giza katika mapito
yangu. Amenivua utukufu wangu, Na kuiondoa taji kichwani mwangu. Ameiobomoa pande zote, name
nimetoweka; na Tumaini langu ameling’oa kama mti”
Ayubu 1:12 “Bwana
akamwambia Shetani, Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini
usinyooshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe, Basi Shetani akatoka mbele za uso
wa Bwana”
Hakuna mtu anayejua
kutenda haki kwa kutenda vizuri.
Kabla ya Yesu kuja
hatukuwa na ufahamu kamili kuhusu Mungu, hivyo lolote ambalo lilifanyika
duniani liwe zuri au baya lilisababishwa na Mungu.
Ayubu 38:1-2
“Ndipo Bwana akamjibu
Ayubu katika upepo wa kisulisuli na kusema, Ni nani huyu atiaye mashauri giza kwa maneno
yasiyo na maarifa.”
Ayubu 40:8 “Je, hata
hukumu yangu utaibatilisha? Utanitia mimi hatiani, upate kuhesabiwa haki”
Ayubu 42:3-6
“Ni nani huyu afichaye
mashauri bila maarifa? Kwa maana nimesema maneno nisiyoyafahamu. Mambo ya ajabu
ya kunishinda mimi, nisiyoyajua. Sikiliza, nakusihi, name nitanena; nitakuuliza
neno, nawe niambie. Nilikuwa nasikiliza habari zako kwa kusikia kwa masikio; Bali sasa jicho langu linakuona. Kwa sababu hiyo najichukia nafsi yangu,
na kutubu katika mavumbi na majivu”
Yesu alitufundisha
maana ya kutubu katika hali ambayo si ya maombi.
KUTUBU ni kugundua na
kubadilika katika maisha ambayo tumekuwa tukiishi
Kuna tofauti ya kuishi
na kuomba toba. Toba sio jambo la kuomba, toba ni jambo la kuishi.
Metamoya ni Neno la
Kigriki lenye maana ya kutubu lenye maneno mawili Metamorphosis
AYUBU NI SAMPLE TU YA
WATU AMBAO WALIFIKIRI WANAMJUA MUNGU LAKINI HAWAMKUJUA MUNGU
Huwezi kutumia 100% ya mawazo ya watu walioishi kabla ya
Yesu kama njia ya kujenga ufahamu bora juu ya Mungu utakaokupa kumjua Mungu kwa
namna ambayo utahusiana naye sawa sawa.
LAKINI KUNA NAMNA ILIYO BORA:
LOOKING FOR A MODEL OF GOD?
Matendo 17:22-32
“Paulo akasimama katika Aeropago, akasema Enyi watu wa
Anthene, katika mambo yote naona ya kuwa ninyi ni watu wa kutafakari sana mambo
ya dini. Kwa sababu nilipokuwa nikipita huko na huko na kuyaona mambo ya ibada
yenu, naliona madhabahu iliyoandikwa maneno haya, KWA MUNGU ASIYEJULIKANA. Basi mimi nawahubirini habari zake yeye ambaye ninyi mnamwabudu bila kumjua. Mungu
aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye kwa kuwa ni BWANA wa mbingu
nan chi hakai katika hekalu…”
GROWING IN THE KNOWLEDGE
OF GOD
Kama humjui Yesu
huwezi kumjua Mungu. Tunaweza kumjua
Mungu bila kupapasa kama wengine walivyokuwa wanafanya watu wa zamani kwa Kumjua
Kristo.
Waebrania 1:1-4
“Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu
nyingi na kwa njia nyingi Mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika
Mwana aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.Yeye
kuwa ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua
vyote kwa amri ya uwezo wake, akiisha
kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa ukuu huko juu...”
Mwisho wa siku hizi
Mungu anasema nasi katika mwana sio kupitia Mwana. Hii ina maana kuwa Yesu
akizizungumza ni Mungu amezungumza.
Siku za mwisho ina
maana ya Siku ambazo Mungu hana mjumbe mwingine tena atakayekuja zaidi ya Yesu.
Alipomleta Yesu alifunga ukurasa. Hatusubiri ishara nyingine ambayo Mungu
ataileta bali Yesu ndiye mfunga na mfungua ukurasa wa siku za mwisho. Agano la
mwisho limefungwa. Siku za mwisho zilianza baada ya Yesu Kristo kufufuka.
“God is in control
enough not to do anything.God is in control in his job description”. Watu wengi
wana nguvu lakini hawwana uwezo wa kujicontrol.
Kinachomsumbua Mungu
ni Upendo wake sio uwezo wake. Uwezo wake humfanya kuwa na nidhamu ya
kutokufanya chochote kibaya kwetu. Ukiweza kitu sio ufanye kila kitu,
YESU ALITUMIA MUDA MWINGI SANA KUREKEBISHA MTAZAMO WAO JUU
YA MUNGU
Yesu alikuwa anaonesha
upande sahihi wa Mungu
Kumjua Yesu ni kumjua
Mungu asilimia 100%
Hakuna maoni: