MOVE WITH MOVERS YOUTH CAMP MOJA YA TABIA ZA MUNGU na Mwl MGISA MTEBE.
MFANO #1: 2Samweli 5:17-25
DAUDI
Nidhamu ya Mfalme Daudi wakati wa
Vita
Daudi alikuwa na nidhamu ya kusikia maelekezo kwa Mungu. Pamoja na kwamba
Daudi alikuwa na Uzoefu bado na nidhamu ya kumsikiliza Mungu.
Sifa za Maelekezi:
Ili kuwashinda Vita hii, Daudi alitakiwa kuwa makini na;
1.
Kuwa Mahali sahihi
2.
Kuwa na watu sahihi
3.
Kufanya kwa wakati sahihi
4.
Kutembea katika Njia sahihi
5.
Kufanya kwa kasi sahihi
Pamoja na Siri za Ushindi tulizo
nazo au uzoefu tulionao bado hatutakiwi
Kuzitegemea Akili zetu wenyewe.
Kiwango cha Mafanikio ya mtu, kinategemea moja kwa moja na Jinsi anavyojua
utendaji kazi wa Mungu.
2Samweli 2:1-2
Ikawa baada ya hayo… (Baada ya hayo YAPI?):- Baada ya Sauli Kufa.
Aina mmbili za mapenzi ya Mungu
1. Permitted will of God (In the cycle of the Will of God)
2. Perfect will of God (At the center of the Will of God)
Waefeso 2:10 | Yeremia 29:13| Walawi
26:27-28
Hautakiwi kuanza kubahatisha maisha. Tayari Mungu ana mipango myema kwetu
tangu awali kabisa.
Usimkariri Mungu, Mungu ana njia
nyingi za kufanya mambo yake.
Yohana 16:13| 14:26
ISAYA 1:19
Changamoto za
Kutekeleza Wito:
1. Muda usio sahihi (Watu na mahali sahihi)
2. Eneo lisilo sahihi (Muda sahihi na Mtu sahihi)
a. People group
b. Location
3. Watu wasio sahihi kutembea nao (Mahali sahihi na Eneo sahihi)
Sio wote watakuwa sahihi kwako, nah ii haina maana kuwa hao wasio sahihi
kwako ni wenye dhambi.
Kila Mungu atakayekupa ana makusudi nawe katika kukusaidia kufika
anapotaka ufike.
Inachukua muda Mungu kuwaandaa Watu kwa ajili yako. Hivyo ni muhimu kuwa
na Nidhamu ya kusubiri na kufuata
maelekezo ya Mungu.
4. Eneo, Muda na Watu wasio sahihi. (Kukosea vyote)
MFANO #2: KUTOKA 24:1-34:35
MUSA
Katika uwepo wa Mungu, Musa alikaa siku 6 akiwa kimya akingoja kumsikiliza
Mungu aseme naye.
Mungu alikuwa anamtengenezea nidhamu Musa ya kuwa Kimya na kuwa tayari
kumsikiliza Mungu. (Nidhamu ya kusubiri.)
Ni rahisi kuwa peke yako umejitenga na watu lakini bado kuna kelele ndani
yako. Moyo wa Musa ulikuwa una kelele nyingi ndani yake kama Kiongozi,a
aliyekuwa na jukumu kubwa la utatuzi wa changamoto za watu.
PRIVACY & SILENCE; Mambo haya yanahitajika sana katika kusikiliza
maelekezo ya KiMungu. Kuna gharama za kuwa Katika utulivu wa kumsikia Mungu.
Kazi ambayo Mungu ametupatia itapimwa kwa IDADI NA UBORA (God’s Standard
are in QUANTITY AND QUALITY)
Mungu anapotaka kutekeleza jambo lolote katika Duniani hufanyika kwenye milango
maalumu ambayo ni:
1.
Milango Eneo mfano Yakobo alipokuwa Betheli
2.
Milango Watu
3.
Milango Muda
Hakuna maoni: