Ads Top

*MIZIZI*



Kama huna mizizi kwenye lolote utang'olewa kirahisi Sana.Mizizi yako imezama kiasi gani kwa Mungu, Kwa neno lake yaani Kristo, kwa Roho Mtakatifu, kwa kuwasaidia wasiojiweza,kwa huduma kanisani , na kwa uwakili wa karama za Mungu? Nini kinakutoa kirahisi kwenye hayo mambo hapo juu? Nini kinakudumaza? Minoxidil haitokei tu kama upepo inajengwa na kuimarishwa kwa mazoezi ya Rohoni na sio six packs, Mazoezi ya mwili yafaa kidogo. *Mizizi Mizizi Mizizi ya imani yangu,* this is for you Raphael and friends.

Mizizi inashikilia mmea na kuulisha ukue. Mizizi inashilia ardhi na kuupa stamina mmea kuwa imara kinyume na upepo na dhoruba. Una stamina katika imani yako? Imarisha mizizi ya ushirika wako kwa Mungu. Zamisha kwa ndani kabisa ili upate stamina ya kukuza mmea

Mizizi iko ndani ya mbegu , Mizizi haipandwi bali mbegu. Mbegu haishikilii mmea Bali mizizi. Mbegu inapandwa kwenye udongo mzuri inazaa 100,60 na 30. Vipi wewe unazaa? Unazaa nini? Vipi ubora wa matunda unayozaa? Vipi kiwango cha matunda unayozaa? *Hizi sio post za ushabiki, ukitaka mabadiliko jibu kila swali, andika , na  chukua hatua.*


Classified Mindset
RAPHAEL LYELA

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.