USIOGOPE, MWAMINI MUNGU NA NENO LAKE UTAKUWA SALAMA
Nakusalimu kwa jina la Yesu ewe Mtanzania popote ulipo!
Ninaandika haya kwa mamlaka ya jina la Yesu!
Najua mengi yapo yanaendelea kutokea na yanaleta hofu, mashaka, wasiwasi na woga mkubwa juu ya hatma ya maisha yetu. Taarifa ni nyingi kuhusu ugonjwa huu wa kuambukiza wa Corona na hofu imetanda duniani. Kwanza ni vema kuchukua tahadhari zote zinazosemwa na Serikali yetu nzuri kupitia vitengo husika, hilo ni la muhimu sana. Lakini pia, mimi nataka niwaambie enyi Watanzania, kwa neno la BWANA MUNGU kuwa USIOGOPE. Hofu ni ugonjwa mkubwa sana kuliko hata virusi vyenyewe. Hofu inapunguza kinga ya mwili kwa asilimia kubwa sana. Ukiwa na hofu chochote kinaweza kukua, hata umeme ukikatika tu. USIOGOPE.
Kutokuogopa haimaanishi usizingatie maelekezo ya Serikali, kumbuka Serikali ipo kwa ajili yako, yaani kukusaidia wewe kuwa salama na hasa kwenye kipindi kama hiki ambacho kila mtu anatamani aongee kitu kusuhu jambo hili. Mungu alimwambia Yoshua, USIOGOPE KWA MAANA MIMI BWANA MUNGU NIKO PAMOJA NA WEWE. Je, huna hakika kuwa Mungu yuko pamoja na Tanzania? Basi USIOGOPE. Japo kwamba maadui wa wanadamu wamekusudia jambo baya kama hili kutokea lakini nakuhakikishia kuwa HAWATAFIKA MBALI KWA JINA LA YESU.
Elewa pia kuwa, Tanzania na Watanznia wote ni mali ya Mungu na ni wajibu wetu kujiweka katika mikono yake iliyo salama kila siku, si tu kwa sababu ya Corona. Hali iliyopo sasa, watu wanaogopa ugonjwa kuliko kuogopa dhambi, kuliko kumwogopa Mungu. Nataka niwakumbushe pia kuwa HOFU YA MUNGU INAONGEZA UCHAJI NA HEKIMA na kumbe ni heri sana kumwogopa Mungu kuliko kuogopa vitu ambavyo havina thamani. Ukiwa unaendelea kufuata maelekezo mbalimbali yanayotolewa, endelea zaidi kumwamini MUNGU na ya kuwa usalama wetu uko mikononi mwake.
Kwa hali yetu kama Watanzania, kwa namna yoyote ile ni mengi ambayo Mungu anatufanyia na kutulinda kwayo bila hata kujua mpaka sasa. Sisi tumekulia kwenye mazingira magumu toka kuzaliwa, CORONA NI NINI? Huku tunachukua hatua mbalimbali lakini tunaikataa hofu ndani yetu na badala yake tukubali Upendo wa Mungu uzidi sana kuishi ndani yetu. Nani ajuaye kuwa mambo haya ni njama au mipango ya hila ya shetani na vibaraka wake binadamu?
Basi usiogope, bali omba. Hili litapita na TANZANIA ITABAKI SALAMA, mimi na wewe tukiwemo. Usiogope kwa kuwa hofu haina majibu mazuri wala suluhisho la maana. Neno la Mungu linasema hivi, JINA LA BWANA NI NGOME IMARA, MWENYE HAKI HUKIMBILIA ILI AWE SALAMA.
Ukiri Wangu: NAIKATAA HOFU JUU YA NCHI YANGU NZURI YA TANZANIA KWA JINA LA YESU, MUNGU IBARIKI TANZANIA NA KILA MTANZANIA POPOTE ALIPO.
By Pastor Raphael Lyela
0744 644699, Dodoma, Tanzania
Mungu akubariki Dady
JibuFuta