Ads Top

KWA KILA MWENYE NIA NJEMA NA TANZANIA NA MAREKANI

 

13/08/2020

Nakuomba uiombee Tanzania na Marekani. Inabidi kuanza kuomba leo, ukiweza kufunga au la ni sawa, kikubwa ni kumuomba Mungu aziepushe hizo nchi mbili na mipango ambayo adui ameikusudia kutokea ndani ya miezi nitakayoitaja hapa chini. Tumuombe Mungu kwamba kama hiyo mipango ni kusudio tu la wanadamu wenye hila basi isitekelezeke na isifanikiwe. Ila kama ni mapenzi yake Mungu na ya kwamba kuna mpango wake kwenye hayo basi Mungu atupe neema ya kusimama imara. Nimeyaweka hayo mataifa mawili kwakuwa yanafanana sana katika kipindi cha miezi nitakayoitaja. Moja wapo kubwa la kujua ni kwamba maisha hayarudi nyuma, hayarudi yalikotoka, kwa mwaka huu wa 2020 mpaka hapa tulipofika hakuna aliyedhani ingekuwa hivi.


Kuanzia mwezi wa Tisa mpaka mwezi wa Kumi na moja, hii ni miezi migumu sana kwa hizo nchi mbili nimezitaja hapa, Tanzania na Marekani. Makubwa ya kufanana ni kuwa nchi zote mbili zitaingia kwenye uchaguzi mkuu wa viongozi wakuu w anchi. Tanzania uchaguzi ni tarehe 28 mwezi wa Kumi siku ya Jumatano na Marekani ni Mwezi wa kumi na moja tarehe Tatu siku ya Jumanne. Hali ya kiroho ya hizo nchi mbili kwa miezi hiyo mitatu haitakuwa salama sana na ndo maana ni vema kuomba rehema za Mungu juu yake. Marekani inatuhusu sana, hivyo usiseme ile ni Marekani. 


Mfalme wa Uajemi amekusudia mabaya juu ya hizo nchi mbili, tusipuuzie wala kusubiri mambo yatokee kwanza ndo tukubali. Tukisubiri yatokee kwanza tutakuwa tumechelewa sana. Huu mwaka wa 2020, Mungu atusaidie kusimama imara. Mfalme wa Sodoma  na Gomorah wamekusudia mabaya. Tusimame imara sana. Niishie hapa kwas asa.


Wako katika Ufalme wa  haki ya Mungu,

Pastor RAPHAEL LYELA

0744644699.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.