TUMIA MUDA MWINGI SANA KUMSHUKURU MUNGU MWEZI HUU WA TISA.
Ni mengi ameshakutendea. Ni mengi ametenda mwezi uliopita. Ni mengi sana kiasi ambacho akili zetu ni ndogo sana kuelewa na kukubali. Akili zetu, hazina uwezo wa kuelewa yote na kuyakubali yote ambayo Mungu ameyafanya maishani mwetu. Akili zetu zina mipaka. Lakini ukweli ni huo, Mungu anastahili shukrani zetu zote kila siku maana kila siku ina siku yake iliyopita ambayo inadhihirisha uaminifu wa Mungu kwetu. Hivyo hivyo kwenye kila wiki, kila mwezi na kila mwaka. Nyakati zote zilizopita, hata kama zilikuwa sio nzuri kwa wakti huo lakini hazikutuua, yaani bado tuna midomo na pumzi basi tunapaswa kushukuru sana. Mshukuru Mungu leo. Mshukuru Mungu kila siku ya mwezi huu wa Tisa. Kusudia kuishi Maisha ya shukrani na sifa kwa Mungu kwa mwezi huu.
Hata kama kuna changamoto unazo sasa, zisikuzuie kumshukuru na kumsifu Mungu wako. Kumbuka, Mungu ameshakutendea mengi mno, amekutendea mambo laki moja lakini wewe umekaa kwenye mambo Matano tu. Mshukuru Mungu kwa kila jambo lilitokea mwezi uliopita, siku iliyopita na wiki iliyopita. Mshukuru sana Mungu leo. Ndio, anza leo na anza wewe. Hakuna mtu atakusaidia kumshukuru Mungu maana hakuna mtu atakaekusaidia kuishi Maisha yako. Hivyo, anza wewe leo. Fungua moyo na kinywa chako na upeleke shukrani kwa Mungu wako.
Huwa unashukuru baada ya kula? Huwa unashukuru baada ya kupewa zawadi? Kwa Mungu ni Zaidi. YOU CAN EVEN THANK GOD IN ADVANCE SINCE HE HAS BEEN THERE FOR YOU ALWAYS. Amekuwa na wewe nyakati na majira yote. Mpe heshima yake. Mungu akubariki sana.
Wako katika utumishi,
PASTOR RAPHAEL LYELA
BALOZI WA KUDUMU WA UFALME WA MUNGU.
Hakuna maoni: