NGUVU YA KUSIMAMA KATIKA NAFASI YAKO-3
...INAENDELEA
ZIPO
DALILI ZA KUONYESHA KAMA UMETOKA KWENYE NAFASI YAKO
Ila kabla
sijazisema hizo dalili, niseme hivi ukishaijua nafasi yako unahitaji nidhamu
kuitunza na kuitumikia hiyo nafasi. Unahitaji ufahamu sana kuitumikia hiyo
nafasi na unahitaji HEKIMA.
Mfano: Mke aliyetoka kwenye nafasi
yake huanza kutaka nafasi ya mumewe na hasa kwenye kufanya maamuzi ya mwisho.
Hivyo hutaka akisema yeye mumewe asiongezee lolote ndo atajiona kupendwa na
kutahaminiwa na hii haimaanishi mke we zezeta hapana ila kuna maamuzi lazima
KIONGOZI aseme,maana makamu wa rais hawezi kuwa rais katika hali ya kawaida.
The same kwa mume.
Mwana mpotevu
alipotoka kwenye nafasi yake,hakuna alichofurahia na akiwe nje ya nafasi yake
asingesikiwa maombi mengine yoyote mpaka alipoomba TOBA,KUGEUKA.
Hata uwe na elimu
kuliko mumeo,bado wewe ni msaidizi mwenye hela kuliko kiongozi.
Hata uwe na akili
kuliko mumeo,bado wewe ni msaidizi mwenye akili kuliko kiongozi wake.
Swala la NAFASI
halibadilishwi kwa elimu au cheo au pesa...lilishwekwa hivo.
Mnalifahamu lile
andiko linaonyesha kuwa maombi ya mume, kujibiwa kwake na Mungu inategemea
anavyoishi na MSAIDIZI WAKE?
Eva asingekuwa
KIONGOZI kwa kujifanya mjuaji.
1 Peter 3:7 tusome
7 Kadhalika ninyi
waume, ishini na wake zenu kwa kuwahurumia, mkitambua ya kuwa wao ni dhaifu na
hivyo muwape heshima, kwa maana ninyi ni warithi pamoja nao wa neema ya uzima.
Fanyeni hivyo ili
sala zenu zisizuiliwe.
Je, tunajua kuwa
NAFASI ya USAIDIZI ya mwanamke ndiyo hiyo hiyo nafasi ya USAIDIZI ya ROHO
MTAKATIFU?
Quotes
by Raphael JL: Kujisahaulisha
hali ulonayo hakuiondoi hiyo hali. Kubali kuwajibika,hakuna malaika atakuja
kukutoa kwenye hali yako kama hauko tayari. Njia rahisi na pekee ya kuukwepa
ujinga ni kujifunza. CHOOSE TO BECOME.
Ushirika
na Mungu!
Usikate tamaa
Usirudi nyuma
Usiache unachofanya
Usikimbie kazi
Usijichukie
Usijihurumie
Usikubali
kudharauliwa kwasababu yoyote ile
Usikubali
kuonekana huna maana
Usikubali
kuonekana hufai
Mkono mwema wa Bwana
ukusaidie
Nakataa kuonewa
juu yako
Nakataa kuonewa
juu ya familia na uzao wako
Nakataa kuolewa
kazini kwako
Naakataa kuonewa
kwenye biashara yako
Hakuna wa kukutoa
kweney nafasi yako
Hakuna wa kukuonea
mbele yako
Usikubali kutoka
kwenye nafasi yako
Usikubali kuacha
wajibu wako
Usicahe shule
Usiache ndoa yako
Kama unajua
hujakosea, usiache....kama unajua umekosea basi tubu
Ugumu haimaanishi
haiwezekani
Kaa kwenye nafasi
yako
Maombi
yanayojibiwa nje ya nafasi ni maombi ya toba tu
Unahama unaenda
wapi?
Mungu akurejeshee
furaha yako
Mungu akurejeshee
tumaini
Mungu akurehemu na
kukufanyia wepesi
Usiache bana.
Usikimbie
Kimbia kama unajua
umemaliza wajibu
Wengine
wanakimbiza pesa wanamuacha mungu bado amekaa anakunywa kahawa
Wengine
wanakimbiza umaarufu na kujulikana
Nakusihi mwana wa
Mungu
Usikurupuke
Furaha ya kweli
iko kwenye nafasi yako
Kama ulimuomba
mungu kupata hiyo kazi au hiyo biashara usiache kwa hiari yako-utateseka sana
Kumbuka ni wapi
ulipokosea, rudi hapo ukaweke mambo sawa
Mungu akutokeeeee
Usiende kwengine
bila Mungu
Usiende peke yako
Usikimbie bila Mungu
Umemuacha Mungu
wapi?
Furaha na amani
iko kwake, ukiwa nae unafurahia
Kila ulichokipata
pamoja na mungu usikiache kwa akili zako mwenyewe au mazingira
Ulipokosea ndo
penye jibu-kubali kuwajibika
Ipo njia
ionekanayo kuwa sawa machoni pako ila imebea uharibifu ndani yake
Stay in your
position
ITAENDELEA...
Asante sana Mwalimu. MUNGU azidi kukupa Hekima. Kwa kweli kmepona. Na Yesu ansaidie kuyaishi haya nlojifunza.
JibuFuta